loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Fifa yaibana TFF

Pia limeitaka TFF kuhamisha ofisi zake za muda zilizopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam na kurejea kwenye makazi yake, Uwanja wa Karume, Ilala ili kusimamia kikamilifu maendeleo ya ujenzi wa ofisi mpya za shirikisho hilo.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Semina wa Fifa, Zelkifli Nguofonja wakati akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kumalizika kwa semina iliyoshirikisha wataalamu wa Fifa na Kamati ya Utendaji ya TFF.

Nguofonja alisema TFF inatakiwa kuimarisha zaidi ligi kwa kuhakikisha kunakuwa na vifaa vya kufundishia na kusimamia uwepo wa makocha wenye sifa kufundisha timu za Ligi Kuu.

Alisema Ligi Kuu ya Tanzania ina msisimko mkubwa ambapo TFF inatakiwa kuendeleza harakati zake za kuifanya iwe bora zaidi.

Alisema TFF imekuwa ikibadilisha ratiba ya ligi mara kwa mara, hivyo kuwataka kuhakikisha ratiba hiyo inaimarishwa na kuwa bora zaidi.

Alisema kwa kuwa na ligi bora, timu ya taifa inaweza kufika mbali na kusisitiza kuwa ili timu ya taifa iwe bora zaidi, inatakiwa ligi kuwa bora pia.

Alisema Tanzania inaweza kuwa katika timu bora 10 za Afrika, lakini hiyo ni hatua inayotakiwa kuchukua muda na sio suala la siku moja.

“Fifa inaridhishwa na utendaji na nia ya kweli ambayo TFF inayo katika kuboresha soka la Tanzania na kuna mengi tumejadiliana nao katika kuhakikisha kuwa mapungufu yanaondolewa,” alisema Nguofonja. Aliongeza kuwa pia wameitaka TFF kuimarisha Kitengo cha Masoko ili kuongeza wadhamini zaidi watakaosaidia ligi hiyo.

Pia aliongeza TFF inatakiwa kuwasilisha kila mwaka taarifa maalumu ya utekelezaji wa miradi yake kwa Fifa, ikiwamo mkakati endelevu wa mwaka mzima wa maendeleo ya timu hiyo.

Katika kuhakikisha kuwa hilo linatendeka, Nguofonja alisema katika kikao chake na shirikisho hilo, wamekubaliana kuwa ofisi zao zihame kutoka Posta na kurejeshwa Karume.

Alisema wakiwa Karume itakuwa ni rahisi kwa TFF kusimamia maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kisasa ambao wamepanga kuutekeleza. Aliongeza kuwa TFF ikirejea hapo ni dhahiri kuwa hata Fifa itakuwa na uwezo wa kuwatambua kirahisi zaidi.

“TFF ina eneo lake hilo la Karume na ni eneo kubwa sana na wakiwa pale hata sisi tutahamasika kuwa tunawatambua kwa uwepo wao kwenye eneo lao na kuwasaidia kirahisi zaidi,” alisema ofisa huyo wa Fifa.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa alisema wataanza kutekeleza agizo hilo hivi karibuni. “Inabidi tuwe na muda kidogo wa kupaboresha pale Karume kwa maana ya ofisi ziwe na ubora zaidi na kisha tutarejea punde tu pakikamilika,” alisema Mwesigwa.

RUVU Shooting, Kagera Sugar na Gwambina ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi