loader
Dstv Habarileo  Mobile
FILAMU: ROYAL DAUGHTERS-Bado inavutia kuiangalia

FILAMU: ROYAL DAUGHTERS-Bado inavutia kuiangalia

Katika filamu hii ambayo naamini storyline imesimama vyema, maisha na mazingira ya mabinti wawili wa kifalme yanaangaliwa kwa makini wakati dairekta akitafuta sababu za kuwapa watazamaji wake kwa nini amemuua mtu ambaye alionekana kujali maslahi ya klifalme hiyo.

Nini hasa dairekta wa filamu hii ametaka kutuambia kupitia waigizaji wake, mzee mzima Olu Jacobs, Ini Edo, Tonto Dikeh, Browny Igboegwu na Joyce Kalu? Katika filamu hii ambapo mabinti hao wa Igwe (mfalme) wanaleta aibu katika kasiri la baba yao kutokana na tabia za kichizi alizokuwa mmoja wa mabinti wale.

Ini Edo ndiye Princess mwenye heshima kubwa lakini yupo mtu ambaye unaweza kusema amechanganyikiwa Tonto Dikeh ambaye hata huo uhuru aliokuwa anautaka alikuwa anautafuta katika njia ya kuua watu waliopo karibu na familia, kwa maneno mengine motto huyu alikuwa na inda yake na nia yake ovu katika mazingira ya kuendekeza hasira isiyokuwa na sababu.

Tangu unaanza kuangalia sinema hii ambayo imerushwa kwa siku mbili tofauti na televisheni ya 1 ambayo inakuja juu unaona kwamba mdogo mtu hampendi dada yake akimfanyia kila vurugu, ili hali dada mtu anampenda mdogo wake kwa kiasi ya kwamba lipotoroka katika kasiri kwa sababu ya kufanyiwa displini aliendelea kumtafuta mpaka pale alipofanyiwa visa vya kuambiwa mdogo wake amekufa na asipige simu, hali iliyomlaza hospitalini kwa kuchanganyikiwa.

Hiyo ni kama haitoshi katika sinema hii kuna kitu kama mzimu kitu ambacho kilimsumbua malkia lakini pamoja na yeye kumsemesha mzee ili waweze kuangalia tatizo lipo wapi mzee alisema ni shida tu ya mawazo. Mdharau mwiba mguu huota tende na katika familia hii kutobadilika kwa Tonto kulisababisha madhara makubwa katika falme, likiwemo la aibu ya kunyweshana sumu.

Tonto alikuwa anaishi maisha yake mwenyewe, ambayo yamejaa ubazazi wa aina kwa aina, ubazazi ambao pia ulimfanya baadae achukue uamuzi wa kumuua dada yake. Aina hii ya maisha ni kama vile anataka kulipiza kisasi cha kutopendwa ingawa kimsingi alikuwa anapendwa.

Labda alikuwa anataka kupendwa na kufanyiwa kama dada yake, lakini kwa kukosa kukua kistaarabu alikuwa amejenga tabia ambayo haikuwa njema kwake, kwa familia na hata kwa nchi waliyokuwa wakiingoza.

Ninaposema storyline imekaa vyema, ni kutokana na ukweli kuwa toka kuanza kwa sinema unakumbana na vitu ambavyo huna majibu navyo mpaka sinema inaisha; na bado sinema imesha ikiwa na maswali muhimu ambayo unaweza kuyatumia kufanyakazi nyingine ya Royal daughters na hapa unaweza kumfanya Ini awe amekufa kweli au afufuke; lakini pia bado haijajulikana.

Yule mwanamke (mzimu) alikuwa na kitu gani na kasiri la akina Jacobs. Aidha kumekuwepo namna bora ya kuelezea upuuzi wa mtoto huyu wa kike ambaye aliwapelekesha wazazi wake kisha kuamua kutoroka wakati wazazi wake walipokuwa wanamtengenezea msingi wa heshima na kupenda wengine.

Tonto alienda kwa rafiki yake wa kike baada ya kusulubiwa na baba yake akimtaka aache ujinga na awajibike. Huko ndiko alikoamua kujiachia kisawasawa.

Aliondoka nyumbani pale, akiacha kizaazaa kwa familia nzima huku dada yake aliyempenda kwa dhati akizimia baada ya Tonto kuwafanyia vitimbi na kudai amekufa baada ya kumpa bwana wake aseme mwenye simu amekufa wakati sikweli. Simu hii aliyozungumza na dada yake , ilimsababisha dada huyo kuzimia na kukimbizwa hospitalini.

Baada ya kumsaka binti yake kwa muda baba aliamua kutoa tangazo lililowatia adabu yeye na rafiki yake na kwa busara ya mvulana mmoja na tukio la baba wa rafiki yake kutaka kurejea nyumbani Tonto alirejea nyumbani. Ambako alilakiwa kama mwana mpotevu akapewa rai kisha akampangia baba yake masharti.

Kabla ya utekelezaji wa masharti inaletwa posa Tonto anaondoka katika posa ile lakini wakati mambo yote shwari anajifanya kupatana na dada yake na kumnywesha sumu. Hakika ni simulizi la mabinti wa mfalme jinsi walivyoonekana kuoneana husuda kiasi ya kwamba mdogo mtu alimuua dada yake ambaye alimtokea tena.

Katika simulizi hatumuoni Ini akifa tunaona wanampepea asubuhi ile aliyolishwa sumu na ndugu yake. Bila kuoneshwa tunakumbana na maelezo wakati mchumba alipokuja kutembelea kwamba mchumba wake yupo hospitalini. Huwezi kusema kwamba Ini amekufa kwa sababu katika mistari yake wakati anamshambulia mdogo wake kwa kumwekea sumu wakati yeye alikuwa anampenda, haikupi njia ya wazi ya kung’amua labda ubabatize.

Alisema atahakikisha anamlinda na kwamba hata wakati anakaribia kufa alikuwa bado anampenda ‘even in my death I love you” hiki kinakufanya umuone dairekta wa filamu hii kama muuaji asiyekusudia na upo uwezekano wa kutoua. Ijapokuwa hakuwa mwazi kama Ini aliendelea kufa au la, tunaachwa pia na wazazi wakihangaika na Tonto hawajui nini kimetokea.

Je, ule mzimu ulikuwa wa aina gani na ulikuwa na shughuli gani na Olu Jacobs ambaye alikuwa akisema muda wote nini alichokosea kustahili adhabu. Wakati mwingine (tunaashumu) yupo hospitalini. Lakini Tonto naye alizimia kutokana na kutokewa na dada yake na kumfokea kwa ubaya aliomfanyia wakati yeye anampenda.

Ni filamu ya mwaka 2010 ambayo niliweza kuitazama tena yote nikifurahishwa zaidi na namna ambavyo dairekta amebaki na maswali yake bila ya mtazamai kuwa na nafasi ya kujua vitu na hata pale filamu ilipomalizika. Ingawa baadhi ya mashabiki wanasema sinema hii ina suck yaani mbaya wako watu ambao wamesema ni nzuri kutokana na simulizi na waigizaji wake.

Unaweza kusema kwamba Tonto alikuwa katika kiwango cha juu kabisa cha ugizaji wakati wa filamu hii na alicheza nafasi yake ya ubazazi kwa namna tamu zaidi na vipande vya kukuweka hoi kama mwanaume vilikuwa dhahiri japo kwa uficho mkubwa.

Ila hakika unaweza kusema katika mazingira ya kawaida mtoto wa Mfalme wa kiafrika hawezi kufa kwa staili ile na kutokana na hili naamini kwamba katika sinema hii dairekta wake katumudu hajaua mtu anakuacha na fikira kamba yupo mtu anakufa.

Kuhusu sanaa iliyomo ndani unaweza kupenda nyumba ya mfalme ambayo imejengwa kama gari la kifahari. Kasoro yake filamu hii ni kwamba kuna kipande kilakula sana muda, kilikuwa cha muziki na kudansi nadhani klabu. Pamoja na kuona viungo vya wasichana wakitisha kwa dansi, mimi naona haikuwa lazima sana au labda walikuwa wanaivuta movie itimie dakika.

MAZAO mengi ya chakula, matunda na biashara kama ...

foto
Mwandishi: Beda Msimbe

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi