loader
Dstv Habarileo  Mobile
FILAMU ZA KISWAHILI: Bado Natafuta- Shamsa Ford this is Lovely!

FILAMU ZA KISWAHILI: Bado Natafuta- Shamsa Ford this is Lovely!

Nikaanza na filamu za kizungu filamu za James Bond, nikaja Fast and Furry kisha nikachukua sinema za kitanzania nikaanza na Danija, nikaja Nipe Nikupe kisha nikamalizia na Bado Natafuta. Naam, niliridhika na Bado Natafuta. Kuna mambo kumbe yanawezekana kwa watu wa kada ya kati kujichana.

Bado Natafuta nimemuona Shamsa Ford, nikampenda, kwani kazi aliyoifanya kama Daktari katika jamii ya watu wenye kipato cha wastani, akiwa kama msichana, akiwa kama mwanamke na akiwa kama mama na misukosuko ya safari ya mapenzi. Kisha niliwaona akina Zuberi Mohammed na Salim Ahmed na mwishoni Patcho Mwamba nikasema raha iliyoje.

Sikuona raha kwa sababu za umaarufu wa Patcho Mwamba la hasha niliona uchezaji uliotulia ambao ulikuwa unacheza na hisia za kikwelikweli, hisia zilizonifanya pia kuikubali skripti kwa kuwa na maneno ya kuudhi na busara papo hapo ikiunogesha kwa namna ya ajabu kabisa filamu hii ambayo hata upigaji picha wake umekuwa bora.

Ni JB akiwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuonesha ukali wake katika udairekta. Aliniudhi sana katika Danija akanifurahisha sana katika Bado Natafuta. Bado Natafuta imesheheni mambo matatu, hasa ubora wa picha na hisia za waigizaji wenyewe. Shamsa akiwa ni daktari Patricia ni daktari kweli na hospitali yake ni hospitali kweli na wagonjwa wake ni wagonjwa kweli.

Katika hili napenda kusema kwamba JB amefanikiwa sana katika kukusanya watu wake waliotoa raha. Kuna ladha mbili tatu hivi za lafudhi ndani ya lugha kwenye sinema hii. kuna usomi, kuna Kichaga na kuna Kimakonde Zuberi na mwenzake Ahmed walahi wanazijua hizo hizo za kienyeji kisha Shamsa na mdogo wake walikuwa kweli na kiefb (kiswaenglish) ambayo ilikuwa inatoka kwa uhakika kuwakilisha daraja la kati la watu walionacho kidogo.

Simulizi hili gongana ni la mapenzi, lakini namna yanavyoumbwa mapenzi katika sinema hii, unaweza kucheka lakini maana yake ilikuwa si bado natafuta, ingawa mwishoni unaweza kuunga. Bado natafuta kiuchumi na kijamii yaani mapenzi. Ni simulizi la daktari Patricia (kwani yeye ndiye mwenye maneno mengi) na Ahmed muuza maji, makenika mwenye bahati mbaya duniani.

Wawili hawa kiukweli wanakutanishwa kwa staili ya kuchombeza, ambayo inakupa kwanza maswali kisha mwelekeo kisha unatenganishwa. Tunaona pati ya kuzaliwa mdogo wake Daktari Patricia na mji hauna maji ya bomba analazimika kuagiza maji kutoka katika mikokoteni.

Hapo ndipo akina Zuberi na Ahmed wanapoingia kazini japo wanagombana na kutokana na uzembe wa mpiga disko Ahmed anapigwa shoti ya umeme na kujikuta anaamka chumbani kwa akina Dk Patricia. Akiwa kijiweni wanasimuliana na kupigana vijembe watu wanamshauri kwenda kutoa aksante ndipo Ahmed akicheza kama James ananunua machungwa kwenda kusema aksante.

Pamoja na kupewa aksante alitolewa baru asiende tena pale. Kama zari, karibu na kwa akina James, Dk Patricia gari lake linaleta matatizo anapoulizia fundi anaelekezwa kwa James kutoka nusura aanguke ndiye yule mtembeza maji. Wawili hao waliendelea kupishana kwa lugha, lakini baadaye wanatengeneza urafiki ambao unakuja kuwafanya waoane na kabla ya mtoto kuzaliwa kuzuka kisanga na kisha James anaondoka kwenda kutafuta.

Miaka saba baadaye, James anarejea mtoto ameshazaliwa anashind- wa kurejea nyumbani kwani kuna mtu ameshachukua nafasi yake anaitwa Bernard nafasi iliyochezwa na Patcho Mwamba. Akitumia mbinu za medani, James anamfuatilia mtoto wake anamfundisha na kumbadili mtoto ambaye anamkubali bila kujua kwamba alikuwa baba yake.

Wakati wanataka kujua kwamba nani amembadili mtoto mpaka anakuwa mwema, Dk Patricia anagundua kwamba ni James. Anamsaka lakini bahati mbaya anamkuta mwanamke aliyekwenda kujigonga kwa James na wanatoleana kashfa. Siku ya kuvikwa uchumba Dk Patricia na Patcho Mwamba kama Benard, James anatokea na ndipo hapo anapotoa ya moyoni kisha anaondoka akimwachia mtihani mzito si tu Patcho , watu na Shamsa mwenyewe.

James anaamua kurejea kwao, lakini Bernard anamrejesha Patricia kwa mumewe na filamu inaisha. Nimesimulia vionjo tu lakini kwenye sinema hii kuna vipande vya maisha unaweza kukoma. Kuna mabadiliko makubwa katika sinema hii hasa staili ya kuunga mambo aidha kuna maeneo ambayo utayapenda, sehemu ya uchungu kuja ghafla baada ya kusoma barua ya James, kwenye pati ya kuzaliwa ile shoti ya umeme, na mwishoni kwenye hafla ya kuvikwa pete Dk Patricia.

Naam, filamu ni nzuri kwa maana kuwa kuna mabadiliko makubwa sana katika utengenezaji wa sinema za Jerusalem. Stori imejengwa katika jiwe ambalo si rahisi kuondolewa na upepo au jua huku bibie Shamsa akionesha kwamba nafasi zile anazimudu kwelikweli. Uchaguzi wa washiriki ulikuwa mzuri, eneo la kufanyia kazi lilikuwa zuri `cut’ zake zilikuwa nzuri.

Tatizo la mwanga si hivyo, mwanga ulienda vizuri hasa rangi zikiambatana na maeneo. Kama tutaendelea kuwa na simulizi za aina hii na waigizaji wa aina hii, lazima tujidai kwamba tunakua na ninakuwa na kila sababu ya kushawishi Watanzania kuzitupia macho simulizi za hapa nyumbani, kwani wapo watu ambao wanaelekea.Je nimpongeze JB?

Naweza kwani nimekuwa nikimfuatilia unaweza kuweka sinema hii na DJ Benny ingawa mwenyewe hakushiriki labda alitaka kama dairekta atengeneze vionjo sawia vinavyotia ladha ya sinema kuwa poa na hili linawezekana kwa dairekta kukazania kuangalia sinema na kuelekeza badala ya yeye naye kushika skripti.

Aidha vitu ambatana katika sinema vimewekwa sawia, na maneno yameenda yanavyostahili. Je nimesifia sana kama wanavyofurahia Wazulu kusifu sana au tuseme kubonga? Hapana, lakini kwa namna fulani nimeona elfu tano yangu niliyoitoa pale Quality Plaza duka la kuuza bidhaa za Steps kuwa halali. Je una la kusema? Nitwangie sms 0713 176 669 au niandikie msimbebeda@gmail.com.

OFISI ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) ni Taasisi ...

foto
Mwandishi: Beda Msimbe

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi