loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

FILAMU ZA KISWAHILI: CHOCOLATE-Utamu wa mapenzi ni tabaka

Chocolate iliunganishwa mahali fulani ukatambua kwamba kweli maisha mithili ya Chocolate yanapatikana katika sinema na pia uraiani, kwani ikiwa imekuwa flavoured creamy ndani ya tabaka ambazo wewe waweza ku crunchy kwa fun, weweh! Nimekupata! habari za Chocolate bana, lazima waisome halafu unasomeka wewe, masihara hayo!

Nilisema awali raundi iliyopita kwamba hii sinema ina jambo kwani raundi ya kwanza pamoja na kwamba tuliambiwa Jacquline Wolper atajitokeza hatukumuona mpaka tunaingia raundi ya pili ambako sasa penzi linaanza kuwa shatashata mwanakwetu na katikati ya raundi ya pili, manake ghafla bin vuu tena bila taarifa Wolper kajaa tele, halafu jamaa anaanza kushangaashangaa, ngoma mbili zimejaa nyumbani kama pishi la udaga halafu zote mbili zinakimbiza.

Ka mchezo wa kuigiza, Mlela kwa jina la Geofrey (sijui kwa nini wenye majina haya wana kidudu hiki-ah nimesema tu usilinganishe kamwe) akatumbua macho kama mjusi aliyebanwa na mlango, akapima akajikuta ikimtoka Jane kisha kamuite na mwenzako (Geofrey anamuagiza dada yake kumuita Aneth) halafu kisigino nenda naye nje hata kabla ya utambulisho... mwe! mbona nakukimbiza aisee ngoja nirejee mwanzo, mwisho mgumu lazima uvumilie na uwe na staha. full stop.

Naam, Yussuph Mlela aliyecheza kama Geofrey alionekana kujali, kujali sana mpaka mama akaenda kula dili na jamaa wa hospitalini ili kiumbe akizaliwa azaliwe still si unajua tena mahali fulani dhamira hii ovu Anneth anaisema wakati anabembelezwa kwa kifo cha kichanga wake kwamba ilikuwa taabu kuwini penzi la jamaa wakiwa wawili lakini akiwa yeye tu anaona mambo yataenda vyema.

Naam mimba ililelewa, ilienziwa na katikati ya safari Mlela akaanza kupenda kweli ha ha ha si unajua tena na dada mtu akaigundua fitna hiyo akamweka kikao kaka mtu, akamwagia upupu kama mtu akawa ngunguri akasema yeye ndiye mwanaume bwana ataamua maisha yake.

Na akome kumfuatafuata na kweli alikoma kumfuatafuata lakini alimwambia vipi Tamla wa kule Uingereza alipoenda kusoma, akasema si kapata mwingine bwana manake hata barua haandiki wala simu hapigi.

Ikafika akajifungua mdada akaua soo akabaki mwenyewe ndipo yalipoanza ya kuanza,mara watu wanaulizana misimamo , mara watu wanadanganyana mara watu penzi hiloooo mara watu wanaletewa chokoleti wanapishana kiswahili ndipo anapoambiwa kwamba yeye ni chokoleti, chokoleti chakula kinachopendwa na yeye amempenda nini kumliza.

Ebwana Jennifer vipande hivi kavipatia kama vile vya mimba, mwanamke analia kweli, pasi shaka kwikwikwi kwefukwefu,hii kali yaani yale mapenzi yaani mimi nimekupenda halafu wewe unanichenjia? nilipenda hapo, nikabaki natabasaaamu naam pale mdada ulicheza yaani zile kwefukwefu sijui ulivuta hisia gani mwanakwetu ha ha ha ha!

Naam kama wanaume wote waungwana Geofrey alisawazisha na kuanzia hapo jamani walikuwa kumbukumbu kisha katikati ya sherehe jinamiza hilooooooooooooo,Wolper akiigiza kamaTamla anaingia nyumbani kwake bila hodi wala karibu , si kwangu bwana! Geofrey macho yanamtoka kwa mshangao lakini si ndio hivyo goma liko bandani sasa wadau hebu fikiria.

Unafyonza ha ha ha haikuwa baridi ilikuwa na majoto. Rachal Haule kaka dada wa Geofrey kwa jina la Jane jinamizi aliilokuwa akimweleza kaka yake hiloo analiona, anakwepeshakwepesha lakini ikambidi kule nje na anneth amweleza jamaa ulikuwa mzigo wake lakini ulipoenda kusoma hakujali mawasiliano.

Tamla alishtuka lakini kaambiwa huyo alikuwa kaazini inakuwaje? Lakini Duh wolper asingependa kama asingelipiga ile mikwara yake anayoizoea, ilikuwa mizito, aliipiga kikwelikweli mpaka Anneth akachanganyikiwa. Manake alisema hawezi kuuza penzi lake kwani li tamu hata kama angelimkuta Geofrey amefunga ndoa hilo varangati lake lingekuwa si la kawaida.

Aneth akadata, ule mdato wa hii haiwezekani, akaenda katika mizunguko akakuytana na Geofrey akasema unajua nakufikiriaje. Umejaa sura ya usaliti. mambo yakawa si mambo akaenda baharini akatufikiri sana unapofunguliwa mlango tupo chyumbani Mlela na Wolper na jamaa akaingia na chuma (Aneth).

Naam hapo ndipo ilipoandikwa ya wazi na Tamla kama aliyepigwa na ganzi alibaki tu anamtazama Geofrey naye akawa kama kapagawa,. Hii inanikumbusha Nabii Suleiman alipowaasa wana wa Israel wasichochee mapenzi katika wimbo uliobora duhh geofrey alikuwa hajui afanye nini , tuyazungumze akaambiwa shut up.

Akapewa chokoleti achukue kwa hiari akakataa tamla, Anneth akaja juu wewe si unataka tushirikiane mwanaume tutashirikiana na ulaji wa chokoleti, na wewe shut up unajua siwezi kuvumilia kukuona unakuwa na mwanamke mwingine... maneno mbele nyuma mbele.. kula chokoleti akasita akamsokomeza mdomoni na chuma mdomoni akaila akamwambia acham ahakikishe kwamba kailam akajua safari tayari haiwezi kurudi nyuma.. haya na wewe Geofrey chukua ule badala ya kula anamuita Jane he na wewe unataka naye ale chokoleti kama wifi yake hapa... macho Jane yamemtoka he he he sikujua kama Jane ana mimacho vile hahaha rachal ulipitiliza pale duh.

Akaona anakataa basiu akaitwaa chokoleti ile akaila hakuchukua dakika naye akaanguka, Mlela akabaki na dada yake na maiti mbili katika kitanda chake na paniki hapa na pale mwishoni pazia linavutwa the End.

Na mimi kwa wiki hii nasema kwaheri ndio ze end jamaa wamejitahidi wanavijikasoro vyao vya kiufundi si muhimu kuliko endelezo la Chocolate, hatukuibiwa kihivyo unaweza kufurahi. Kumbe mapenzi ni sawa na Chokoleti yanatesa halafu kuna tabaka kwa tabaka za utamu, utamu ....

TANZANIA imeridhia mikataba na matamko mbalimbali ya kimataifa yanayotoa haki ...

foto
Mwandishi: Beda Msimbe

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi