loader
Dstv Habarileo  Mobile
FILAMU ZA KISWAHILI: JB, Kanumba, Niva watesa 2013

FILAMU ZA KISWAHILI: JB, Kanumba, Niva watesa 2013

Kauli hiyo nimetolewa na ofisa mmoja wa Steps Entertainment, Kambarage wakati akizungumza na gazeti hili juzi. Alisema pamoja na wakongwe kupishana kwa hatua chache, chipukizi Niva amekuja juu kwa sinema zake za Gubu la Mume na Tabu ya Kuolewa.

Alisema Steps ambayo ina maprojuza takribani zaidi ya 15 wanaofanya nao kazi, soko lao lipo taiti kutokana na mazingira yalivyo ingawa upenzi wa sinema miongoni mwa Watanzania unazidi kuongezeka.

Alisema wanapofunga mwaka Steps inaona kwamba tasnia inafanya vyema na hasa chipukizi ambao wamekuwa wakitoa sinema zenye kulingana na matakwa ya wananchi, yaani sinema zinazoangalia maisha ya kawaida ya Watanzania.

Amesema pamoja na mafanikio yao wanadhani kwamba serikali bado ina jukumu kubwa la kusaidia uimarishaji wa sekta kutokana na sehemu kubwa kukwamishwa na watendaji wake ambao wamekuwa wakisema wazi kwamba zile ni ofisi zao.

Alisema mwenendo wa polepole wa bodi ya filamu nchini kunafanya kazi ya uzalishaji sinema kuwa kama kitu binafsi cha bodi wakati yenyewe kuwepo kwake ni kuwasaidia wasanii kutanua zaidi katika sekta yao. “Mathalani nikuambie sinema ya Rwanda Genocide imechukua mwaka kupata kibali huku sinema kama ya Spice Island imekataliwa kuingia sokoni kwa dai kwamba inawakumbusha watu majonzi,” alisema kambarage.

Steps ambao ni wasambazaji wa sinema wanasema kwamba kuwapo kwa bodi kunatakiwa kuwasaidia wasanii na wao katika kuhakikisha kwamba tasnia ya filamu inakua, hasa kwa kuzingatia kwamba taifa hili lipo katika mabadiliko makubwa sana ya namna ya kuishi na kueneza ustawi wake wa kijamii.

Pamoja na kuelezea sinema za Shikamoo Mzee na Love and Power kufanya vyema amesema kwamba, filamu nyingi zingelifanya vyema kama vikwazo kadhaa vya kiufundi, kiutendaji na kiuendeshaji kitaifa vingeondolewa.

Pamoja na kuilalamikia Bodi ya Filamu kwa yenyewe kuondoa uhuru wa mawazo ya wasanii badala ya kuyawekea madaraja na kutaka wazalishaji wafanye wanavyotaka wao, kwa sheria ambayo inaonekana ni ile wakati wa uchumi wa kijamaa, mwenendo wa bodi unaleta dhiki kwa wazalishaji na kuleta hasara kubwa kwa wasambazaji ambao mara nyingi ndio wanaotoa fedha za kuzaluisha sinema.

“Hata hawa wazalishaji (maprojuza) wamekuwa na shida kubwa wamekopa fedha kuzaliusha sinema, halafu mtu mmoja anasema hii sinema isiingie dukani kwa kuwa itawakumbusha wtau majonzi. Nini maana ya sinema? “ alihoji Kambarage kama Kambarage.

Akizungumzia juhudi za serikali kukabiliana na uharamia kwa kutoa stika alisema kwamba katika mazingira ya kawaida, inaonekana inafaa lakini stika hizi nazo zina shida nyingine, zinatakiwa kununuliwa kwa fedha za kigeni paundi.

Alisema hajaelewa kwa nini yeye anunue stika kwa fedha za kigeni wakati lengo la serikali ni kusaidia kuzuia uharamia wa kazi za wasanii, lakini pamoja na hayo alisema kwamba stika zenyewe ni shida kuzipata. Hata hivyo, shauri la stika bado ni mjadala kwani mmoja wa wasanii alisema kwamba wasambazaji wanahaha na stika kwa sababu zao binafsi kwani serikali inataka stika kupewa mzalishaji halisi wa sinema .

Pia ameilalamika Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kwa kutoa vibali kwa waonesha sinema (vibanda) na wenye magari ambao huonesha sinema bila kununua kazi nyingi huku, durufu wanaoitumia ikiwanyima fedha wasambazaji. Aidha wapo watu wenye kompyuta zao ambao wamepewa kibali cha kuunguza CD na hivyo kuwa shida sana.

“Tatizo jingine katika mauzo lipo kwa televisheni za kebo. Televisheni hizi zinaonesha sinema zikisema zina kibali kutoka TCRA lakini hakuna kanuni za rejea zinazoonesha kwamba wao wanaruhusiwa kuonesha sinema. Kuna tatizo la hatimiliki hapa na serikali lazima itusaidie.”

Alisema katika mazingira ya kawaida alisema Kambarage soko lipo lakini uingizaji wa sinema kutoka nje bila ushuru kunadumaza uzalishaji wa Tanzania na wasanii kukosa mapato kwa kuwa wengi wa watu wanaona bure sinema kwa gharama ndogo zaidi kupitia mabasi na kebo.

OFISI ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) ni Taasisi ...

foto
Mwandishi: Beda Msimbe

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi