loader
Dstv Habarileo  Mobile
FILAMU ZA KISWAHILI: MKONO WA MUNGU-Uchawi wake kidogo unaeleweka

FILAMU ZA KISWAHILI: MKONO WA MUNGU-Uchawi wake kidogo unaeleweka

Ukiangalia sinema hii kwa makini, Mkono wa Mungu umecheleweshwa sana, lakini washiriki wake wamefanya vyema, kwani si majina makubwa yaliyosheheneza sinema hii bali watu wapya ambao wamefanya vyema katika nafasi zao huku bi mchawi kama kawaida yake akiwa na nafasi kubwa ya kuonesha umahiri wake katika nafasi hizo.

Mkono wa Mungu unapata nafasi ya kuonwa mwishoni, lakini awamu ya kwanza yote unaona vituko vya mirathi ya hatari kama unaweza kuiita hivyo. Naam, nasema ni mirathi ya hatari kwa kuwa msingi mkubwa wa matatizo ya staa wa filamu hii ni mkoba wa babu yake, mkoba ambao ulikuwa na zana zote za maangamizi katika dunia ya kiza.

Naam, msomi anakabidhiwa mkoba, anaukataa wakati ulipofika na anasema hovyo sana. Katika sinema hii salamu za nini kilitokea mpaka kijana staa anakuwa na misukosuko mingi unaikuta karibu na mwisho. Ingawa tunaanza na majonzi kwa maana ya kwamba ofisi inamkaribisha mtu aliyetoka kumzika babu yake.

Wakati akirejea taabu ikaanza kwa ndoto za kutisha za kutishia mauaji yake, wanakorofishana na mchumba wake, anatuhumiwa uchawi ofisini na mwishoni mwa siku anafukuzwa na kurejea nyumbani kwao. Huko anafumbuliwa kwa nini anapata shida, mjomba wake na shangazi yake wanazungumzia dhiki imesababishwa na nini.

Kama vile ufalme hauwezi kufitiana, kijana anapata shida kubwa, shida ambayo inatokana na kugomea mkoba ule na hasira ya wachawi kutaka kuurithi mkoba na yeye kutaka kumtoa kafara.

Naam, mtengeneza sinema Athumani ameonesha dhahiri kwamba anajua anachofanya ingawa ujumbe wa mkono wa Mungu unadhirishwa mwishoni kwa maana ya kwamba mtu kupita katika misukosuko ni kitu cha kawaida katika maisha Magumu kwani ni sehemu ya fursa ya kuuona mkono wa Mungu.

Staa, kwa hiyo tabu alipata taabu ili aweze kumjua Mungu, lakini katika hili hakumjua Mungu, Mungu alimjua yeye wakati alipofungwa na sihiri asiweze kuondoka eneo lile. Katika sinema hii haikuoneshwa tangu mapema suala la imani kwa Mungu kwa kila jambo lakini tunaona kwamba Mungu kwa namna ya ajabu kabisa aliweza kumchomoa Sagil katika dhiki yake na yeye kupata fursa ya kuwa huru.

Ni ukweli kuwa uso wa Mungu haujifichi unapomwita kwa imani, katika sinema hii aliokolewa kwa rehema za Mungu na wala si kwa tafakari zake kwani yeye alikuwa anamlalamikia babu yake kwanini anamfanya hivyo wakati Mungu alipomuita kutoka uwinguni wakati amefungwa kisihiri.

Naam alinasuliwa pale akatembea akavuka mito mikubwa na kulikuta taifa la Mungu kanisani, wakamuombea, na uchawi na koba lile ukauguzwa na moto wa Mungu na yeye akapewa Biblia kama rafiki mwenzi wa msaada filamu inaisha hapo bila kutuleeza kama alirejeana na mchumba wake au alirejea kazini.

Nimesema tangu awali nataka kuzungumiza uchawi katika sinema hii. pamoja na kuchukua mfumo wa uchawi wa Nigeria, kidogo kuna mabadiliko kwani uchezaji wa uchawi umeboreka kidogo. Kuna mambo kadhaa yanayoonesha kupanda kwa utaalamu wa kuigiza uchawi, ingawa kuna eneo limefanyiwa chuku sana.

Niseme tu kwamba waigizaji walijitahidi, na dairekta alijitahidi kuweka kidogo mambo sawa ingawa usiku ulimtia kasoro. Lakini katika hili nampenda Jengua alitulia sana na Grace Mapunda pia alikuwa mama wa kijijini.

Uchawi uliofanyika, ulikuwa na maana kubwa kwa kuwa ulionekana dhahiri kwamba yapo mazingaombwe, lakini ukakosa mfumo wa uchawi wa kibongo kwani wabongo uchawi wao haujengewi vibanda, kama ni kijini tunajua ni nyumba ya nyasi na kitisho ni vibuyu na hirizi kwani huyu mganga chimbua hatumii vitabu kufanya kafara zake.

Lakini jingine ambalo limetia kiwi ya akili ni kule kanisani, staa alifanyakazi sana lakini nadhani mwandishi wa skripti alikosa maneno stahiki ya wapunga pepo , watumishi wa Mungu kwa staili ya ulokole. Pamoja na kasoro ndogo ndogo Mkono wa Mungu wahusika waliitendea haki hasa wale wakubwa. Kwa leo tuachie hapa napatikana msimbebeda@gmail.com au sms 0713176669 kwa pamoja tutanyanyua sanaa yetu ya uigizaji Tanzania.

OFISI ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) ni Taasisi ...

foto
Mwandishi: Beda Msimbe

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi