loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

FILAMU ZA KISWAHILI: ROOM 13-Nimeiona ZIFF Hadithi ya majini ambayo haina mashtaka

Ni filamu ambayo ukiitazama utaona kwamba imepigwa eneo moja na hivyo kupunguza gharama, lakini pia kuinyima nafasi ya kutanuka zaidi. Simulizi la sinema hiyo limelala zaidi katika dhamira ambayo imewekwa kupitia mzimu wa mwanamuziki aliyekuwa anawania na kulazimika kuishi katika chumba alichopewa mwanzo mpaka alipotoa albamu.

King Majuto ambaye jina lake halisi ni Amri Athuman, amefanya ununuzi wa hoteli. Anaanzisha biashara ya hoteli, lakini hakuwa anaelewa kwa nini chumba namba 13 hakipangishwi. Maelezo yaliyotolewa yalikuwa chumba namba 13 kina mzimu, kauli ambayo Majuto aliikataa na kwenda katika chumba hicho akapata trela, lakini akaamini kwamba ni mawazo yake tu.

Raundi ya kwanza ya sinema hii inaonesha zaidi kazi, hosteli na vijana wawili wenye matatizo ya kikazi katika mfumo wa komedi. Wafanyakazi wawili wanakubaliana kwamba kuna mzimu katika chumba namba 13 na mzungu mmoja jeuri mwenye maneno ya kashfa alijikuta akikimbia kutoka katika chumba hicho baada ya kushindwa kuukabili mzimu wa mdada huyo.

Kelele zake na mbwembwe hazikufua dafu, kwani alitoka mkuku na chumba hicho kubaki na simulizi la kuwa na mwenyeji mzimu. Mzimu huo unaopenda kuimba ulienda sambamba na mgeni mmoja mwenye matatizo makubwa ya kifedha, Peter ambaye baadaye anamsaidia kurekodi ndoto yake na kwenda mbinguni.

Mtengeneza sinema wa Room 13 Amitabh Aurora amesema waigizaji wake wengi ni wa Zanzibar na kwamba alikuwa na kazi kubwa ya kutengeneza sinema hiyo katika kipindi cha siku 10. Aurora ambaye tayari ana filamu tano amesema lengo la kufanya sinema hiyo ni kuendeleza simulizi za kiasili zinazothaminiwa.

Pamoja na gharama filamu ya Room 13 ambayo inazungumzia kujituma hadi kifo, imetengenezwa katika mfumo ambao unapata majibu ya nini kimesababisha mzimu wa Maunda katika awamu ya pili. Unapoanza sinema hii unaona mazingira ya Zanzibar na unaona simulizi taratibu linajipa hasa pale mzungu jeuri anapojikuta anafanyiwa visa.

Sina uhakika matusi yale ya kikoloni yalikuwa na sababu gani, lakini ninajua kitu kimoja kama ndivyo ilivyo dharau yake si ya kawaida na haina maana yoyote. Mzungu aliondoka, maana yake nini Aurora, kwamba wazungu wanawatusi waswahili? Sina uhakika ile ni dharau mbaya kabisa katika maisha haifai.

Pamoja na hayo tunaona jinsi mambo yanavyokuwa magumu katika simulizi hasa upigaji picha wa jini na watumishi wa ndani ya hoteli Pateli na Papi. Mzungu kabla ya kukimbia waliwashana maneno ya kukatishana tama ya muziki kati yake na mzimu na alipotaka kuupiga alijikuta anapigana na vitu vingine kabisa na kuamua kukimbia.

Mzungu aliambiwa anapiga kelele na si muziki na yeye akawa na majibu yake yanayoudhi. Maunda amefanikiwa kuicheza nafasi yake hasa alipokutana na Peter kwanza aibu na pili aliweza kumshawishi kukubaliana naye kumsaidia yeye amalize kazi yake na kisha arejee mbinguni.

Watu waliteseka walipoingia namba 13, lakini Peter hakuteseka; walifika wenye ndoa wakaondolewa bila kuelewa, lakini katika mazingira ya ajabu kabisa Peter alisimuliwa visa na Maunda akabaki anashangaa na kuondoka. Peter akiwa na matatizo makubwa ya fedha analazimika kukubaliana na plani ya maunda ambapo alisema dawa ni yeye kumuingia kisha watengeneze albamu.

Walitengeneza albamu ilihit ikamaliza madeni ya Peter na kumrejesha mbinguni Maunda ambaye aliomba ruksa kwa baba yake abaki ili amalize kutengeneza albamu. Baba wa Maunda nafasi iliyochezwa na Hashim Kambi ni ya dakika chache lakini imeonesha kwamba mzazi naye hamjui mtoto na pamoja na kutomjua alimpa uhai wa kuendelea kuishi mpaka atakapopata nafasi ya kumaliza kurekodi albamu yake.

Alikuwa anaweza kufanya hivyo kwa kumpata mtu ambaye atakubali aingie kwake na kufanya naye kazi pamoja. Alikuwa na wakati mgumu lakini mwishoni aliweza kumpata wa kumsaidia. Kimsingi, hadithi inaeleweka na kuna vijichekesho vya majuto na mtu aliyejiita Pateli lakini kuna maudhi ya matusi kutoka kwa mzungu na pia kukosekana kwa upanuzi wa unaostahili wa hadithi ili kuipa urefu unaostahili.

Nataka kusema kama uhariri ungelifanyika vyema sinema hii inafaa dakika 15, samahani kwa kusema haya kwani pamoja na kumpenda Maunda na muziki wake, baadhi ya scene alizopewa mistari mingi hazikuwa na maana.

Hadithi lazima itoe funzo fulani, ukitazama Room 13 haina faida sana inayoonekana katika akili maana yake ni wazi ni simulizi tu lililokatishwa, kwani muuaji haadhibiwi na mafanikio ya Peter hayaoneshwi wazi huku familia yake ikiwa haijulikani.

Vifereji vya sauti ni vya muziki wa nyumbani lakini maisha yanayooneshwa ndani si ya kawaida kwani pamoja na kuonekana Hashimu baba aliyekufa amekuja kumchukua mwanawe mwisho wake ni mgumu kuliko mwanzo wake.Vipo vituko vya majuto, lakini vyenye ucheo katika daraja la maisha, ni mfanyabiashara mkali.

"The Game Changer: President Magufuli's First Term in Office" ...

foto
Mwandishi: Beda Msimbe

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi