loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Flaviana Matata ahimiza uboreshaji elimu

Matata alisema tangu taasisi yake ianze rasmi Oktoba mwaka jana, imekuwa ikifanya kazi ya kuhamasisha, kuwezesha na kusaidia wasichana nchini kwa kuwaelimisha na kuwapa misingi ya kuwajenga kuwa kati ya watendaji wazuri wanaochangia katika shughuli za maendeleo ya jamii.

“Ili kufanikisha hayo, FMF inawadhamini wanafunzi wasichana kwa kuwalipia ada za shule, kuwanunulia sare za shule pamoja na misaada mingine mbalimbali yenye kumwezesha mwanafunzi kusoma vizuri kuanzia elimu ya upili na hatimaye kufikia kwenye taasisi mbalimbali za elimu ya juu,” alisema Matata.

Matata alisema mapato yanayotokana na mradi huu yanatumika katika kulipia ada, kununua sare za shule pamoja na gharama nyingine zinazohusu na kuwapatia elimu bora ambao wapo chini ya taasisi yake.

Alisema mpaka sasa tayari imewafadhili wasichana 15 wanaosoma katika shule mbalimbali za sekondari Tanzania chini ya ushirikiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF ambao wamekuwa wakishirikiana kwenye mradi wa “Back to School Project” katika kutimiza malengo yake ya uwajibikaji kwa jamii.

Alisema PSPF wamesambaza vifaa vya shule vinavyojumuisha begi moja la shule, madaftari ya mazoezi 12, mkebe mmoja, kalamu za wino tatu, kalamu za risasi mbili, na ufutio mmoja ambapo katika awamu ya kwanza ya mradi ulianza mwezi huu wamechangia vifaa 1,000 kwa wanafunzi wasiojiweza mkoani Pwani.

“Wanafunzi 280 wa Shule ya Msingi Chanzige - Kisarawe, wanafunzi 420 wa Shule ya Msingi Kimanzichana - Mkuranga na wanafunzi 300 wa Shule ya Msingi Msinune Bagamoyo wamepokea vifaa vya shule kwa muhula wa masomo 2014. Tunatarajia kuwafikia wanafunzi wapatao 1500 na zaidi Tanzania wakati wa awamu ya pili ya mradi mwezi Julai, 2014,” alisema.

Katika hatua nyingine, Russell Simons ambaye ni mfanyabiashara mashuhuri na mwanaharakati, aliyemtambulisha Flaviana Matata katika fani ya uanamitindo nchini Marekani, amechangia madaftari ya mazoezi na kalamu za wino kwa watoto wasiojiweza 500 walio chini ya Tanzania Mitindo House Dar es Salaam, The Olevolos Project, Arusha na Shule ya Msingi Mwasele mkoani Shinyanga.

Kila mwanafunzi atapokea madaftari ya mazoezi 12 pamoja na kalamu za wino mbili.

TIMU ya Ruvu Shooting imeboresha kikosi ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi