loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Flyadubai kufanya usafiri Dar, Z’bar

Uanzishwaji wa njia hizo zitakazozinduliwa rasmi hivi karibuni, kunatajwa ni sehemu ya mikakati ya shirika hilo kupanua mtandao wake katika njia ya Afrika Mashariki.

Taarifa ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, Ghaith Al Ghait aliyoitoa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, safari hizo zitaanza rasmi kuanzia Oktoba mwaka huu na kukuza mtandao wa shirika hilo la ndege barani kwa kuwa na vituo 12.

Alisema nauli ya kwenda na kurudi kutoka Dar es Salaam hadi Dubai itaanzia dola za Marekani 399 ikijumuisha mzigo wa kilogramu 20 uliokaguliwa.

Alisema Tanzania ni kitovu cha utalii wa Afrika Mashariki ambapo mwaka jana pekee nchi hiyo ilikaribisha watalii takribani milioni moja kulingana na takwimu zilizotolewa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka mara mbili ifikapo mwaka 2017.

Makamu Mkuu wa Rais wa Biashara wa shirika hilo, Sudhir Sreedharan alisema mtandao wa anga wa shirika hilo Afrika unaoendelea kukua na hivyo kuunga mkono Dira ya Utalii ya mwaka 2020 ya Dubai inayolenga kuvutia wageni milioni 20 katika Umoja wa Falme za Kiarabu.

Aidha alisema Tanzania ni nchi inayojulikana kwa uzuri wake wa asili na wanyamapori ambapo pia Dar es Salaam ni kitovu cha biashara nchini humo na ni mji wenye bandari inayovutia biashara, kuna vivutio pia vya kitamaduni na kihistoria.

Alisema Unguja, inayojulikana kama Kisiwa cha Viungo, imefunikwa na pwani nyeupe na imejaa utamaduni, historia na wanyamapori wanaopatikana huko pekee.

Hivi karibuni Flydubai ilitangaza uzinduzi wa safari za ndege za Bunjumbura nchini Burundi, Entebbe, Uganda na Kigali, Rwanda na safari za vituo hivi zitaanza mwishoni mwa mwezi huu.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi