loader
Dstv Habarileo  Mobile
Gari la Rose Muhando lakamatwa

Gari la Rose Muhando lakamatwa

Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Enock Lukumbo alisema walipokea maagizo kutoka Mahakama ya Mkoa ya kukamata gari hilo kutokana na madai ya mdeni wake aliyemtaja kuwa ni Andrew Nyaki anayemdai msanii huyo kiasi cha Sh milioni 13.

Kesi hiyo ya madai ni namba 4 ya mwaka 2014 iliyotokana na kesi ya msingi ya madai namba 25/2014.

Lukumbo alisema, takribani majuma matatu yaliyopita walipatiwa amri hiyo na mahakama, lakini hawakufanikiwa kukamata gari hilo hadi mwishoni mwa wiki (Ijumaa) walipokuta gari hilo likiwa limeegeshwa maeneo ya Barabara ya Iringa na kulikamata.

Amri ya mahakama ya kukamata gari hilo ilitolewa Mei 5, mwaka huu kupitia barua ambayo gazeti hili ina nakala yake. Gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser – Prado lenye namba za usajili T484 BEB.

“Tulipata taarifa gari hilo likiwa eneo la Barabara ya Iringa, lakini baada ya kufika Rose hakuonekana na baada ya gari lake kukamatwa tulipompigia simu hakutaka kupokea na ndio maana tukaamua kuondoka na gari kwa sababu ndilo tulitakiwa kulikamata,” alisema Lukumbo.

Alisema kwenye kesi hiyo iliyosababisha gari kukamatwa, msanii huyo alikuwa akidaiwa Sh milioni 13 na mdai wake, Nyaki, lakini sasa kutokana na gharama za kumtafuta zitakuwa zimeongezeka.

“Hatujui mahakama itasemaje kwani kipindi cha Sikukuu ya Pasaka tulimtafuta Morogoro na kufanikiwa kupata gari hilo, lakini kutokana na kutopata ushirikiano, tulikwama kulichukua gari hilo,” alisema Lukumbo na kuongeza kuwa gharama halisi, mahakama hiyo itaamua zaidi.

Hata hivyo, Muhando alipopigiwa simu yake ya mkononi alikataa kuzungumzia sakata hilo, kwa madai kuwa yeye hajui kama gari lake limekamatwa. “Mimi sijui kitu chochote kama gari langu limekamatwa na kampuni yoyote na nakuambia sijui sijui,” alisema na kukata simu.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi