loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Gari lagonga watoto 9

Watu hao walipata majeraha mbalimbali mwilini. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema jana liliacha njia na kugonga watu hao katika Barabara ya Pugu eneo la Gongo la Mboto, Mwisho wa Lami.

Majeruhi hao ni Pendo Tilya (32), ambae ni mfanyakazi wa Pepsi aliyekuwa ndani ya gari na amelazwa Amana.

Wengine waliotibiwa na kuruhusiwa ni Hadija Kasim(16), Irene Gabriel (13), Asha Omar(13), Nusura Mbaga(14), Nonda Adam(10), Shedia Abdul(10), Narda Omar(12), Rukia Ally(14), Rehema Said (15) na Among Abdu.

Alisema gari hilo lililokuwa likitoka maeneo ya Pugu Sekondari kwenda Uwanja wa Ndege, lilipofika maeneo hayo lilimshinda dereva na kwenda kugonga ukingo wa barabara na kisha kukosa mwelekeo na kuwagonga watembea kwa miguu kumi pembezoni mwa barabara.

Watu hapo walijeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao na kutibiwa katika hospitali ya Amana. Katika tukio lingine, muuza maji na mkazi wa Mburahati Mianzini, Waziri Kobelo(21) amekufa papo hapo baada ya kunaswa na umeme.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema kifo hicho kilitokea juzi asubuhi ambapo kijana huyo wakati anapita njiani alinaswa ghafla baada ya kukanyaga nyaya za umeme zilizokuwa zimeanguka maeneo hayo.

Alisema nyaya hizo zilikuwa uchi na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala.

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: Hellen Mlacky

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi