loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hafidh Badru kocha mpya Taifa Stars

Badru aliwahi kuwa kocha wa Stars mwanzoni mwa miaka ya 2000. Mara ya mwisho alikuwa kocha wa Polisi Zanzibar inayoshiriki Ligi Kuu ya huko kwa sasa.

Taarifa za ndani ya TFF zilizoptikana Dar es Salaam jana, zilisema kocha Badru ataongoza kikosi cha Stars kitakachokwenda Windhoek, Namibia, Machi 3 kucheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya huko.

“Kocha Badru ni wa muda tu atakuwa na timu katika mechi ya Namibia kabla ya jukumu hilo kupewa kocha mpya, na Badru atakuwa na kocha wa makipa Juma Pondamali,” alisema mtoa habari wetu ndani ya TFF.

TFF inadaiwa kusitisha mkataba wa kocha wa sasa, Kim Poulsen na ipo kwenye hatua za mwisho kumpa kazi hiyo kocha raia wa Uholanzi.

Jana Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alituma kikosi cha wachezaji 22 walioitwa kuunda timu ya taifa kwa ajili ya mechi hiyo iliyopo kwenye kalenda ya Fifa.

Kwa mujibu wa Wambura, timu hiyo itakwenda Windhoek, Namibia, Machi 3 kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa mjini Windhoek Machi 5.

Wachezaji walioitwa katika timu hiyo ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Simba) na Mwadini Ally (Azam).

Mabeki wa pembeni ni Edward Charles (JKT Ruvu), Erasto Nyoni (Azam), Hassan Mwasapili (Mbeya City) na Michael Aidan (Ruvu Shooting).

Mabeki wa kati ni Aggrey Morris (Azam) na Kelvin Yondani (Yanga) wakati viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), David Luhende (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Jonas Mkude (Simba) na Mwinyi Kazimoto (Markhiya Sports Club, Qatar).

Washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance Mwanza), Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Yanga), Ramadhan Singano (Simba) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).

Aidha, katika taarifa hiyo Wambura alisema wachezaji ambao timu zao zinacheza mechi za mashindano ya kimataifa na ligi wikiendi hii wataripoti kambini mara baada ya mechi zao kumalizika.

KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi