loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Haijafahamika kwa nini gridi ilizimika

Hayo yalisemwa jana na Kaimu Meneja Uhusiano Tanesco, Adrian Severin. Alifafanua kuwa kitendo hicho, wanakichukulia ni dharura ambacho ni nadra kutokea kwa gridi yote kuzima.

Alisema umeme ulikatika juzi saa 1.19 usiku baada ya gridi ya taifa, kuzima na hivyo kusabisha nchi nzima kukosa umeme na kurejea saa 4:48 usiku nchi nzima, baada ya kuwasha mashine zote bila tatizo kuonekana.

Alisema kutoka kwa gridi ya taifa, kuna sababu mbili kuu, moja kama kukitokea hitilafu ya mmoja ya mitambo ya kuzalisha umeme mfano Kidatu, Mtera, Kihansi, Hale, New Pangani, Nyumba ya Mungu, Ubungo 1 & 2 au Tegeta gridi inaweza kuzima.

“Yaani kwa lugha rahisi ni kwamba mitambo yote ya kuzalisha umeme, inabeba mzigo mmoja, kama mtambo mmoja ukizima , unasababisha ombwe ambapo mitambo inayobaki inashindwa kuubeba na hivyo nayo kuachia mzigo na hatimaye mashine zote hutoka (huzima),”alisema.

Severin alisema sababu ya pili, mitambo ya wateja wakubwa kama vile migodi na viwanda vikubwa vya uzalishaji, wateja hao wakubwa mitambo yao ikipata hitilafu na kuzima ghafla, inaweza kusababisha mfumo wa gridi kuzima kwa mtindo huo huo wa kuzidiwa kwa mzigo kwa mitambo.

Alisema kwa nchi nyingine, gridi haiwezi kuzima kwa kuwa wanazalisha umeme wa ziada.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi