loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Hakikisheni kila anayefika la saba anaenda sekondari-JK

Pia alitaka viongozi na maofisa elimu kuwafuatilia wanafunzi wanaoacha shule wanakwenda wapi kutokana na kuwa na mdondoko mkubwa wa wanafunzi wanaocha shule za msingi.

Alisema hayo jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara Mpwapwa mjini. Alisema wazazi na walezi wanatakiwa kuhakikisha kila mtoto anayefika darasa la saba anakwenda sekondari.

“Tunataka kutoa fursa kwa watoto kupata elimu ya sekondari na Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu, vitabu,” alisema. Alisema sasa Serikali imetoa Sh milioni 500 kwa halmashauri ili kujenga nyumba nyingi za walimu kwa wakati moja.

Pia alitaka viongozi kufuatilia watoto walioanza darasa la kwanza ambao hawakumaliza elimu ya msingi. Alisema kumekuwa na tatizo kubwa la mdondoko wa wanafunzi kwani wanaoandikishwa kuanza darasa la kwanza ni wengi lakini wanaomaliza darasa la saba ni wachache.

“Viongozi wengi hawafuatilii wanafunzi wanaoacha shule wanakwenda wapi, maofisa elimu nao hawajiulizi katika hili wanaangalia kiwango tu cha ufaulu lakini hawafuatilii kwa nini wanafunzi wengi wanaacha shule’ alisema.

Alisema ni lazima kujiuliza idadi kubwa ya wanafunzi wanaoacha shule wanakwenda wapi ili ijulikane kama wameolewa.

“Mtoto wa kike anatakiwa kuwa darasani na si kuwa mke wa mtu lazima mwanamume huyo akamatwe apelekwe mahakamani huyo ni mbakaji,” alisema.

Mkuu wa Wilaya, Gift Msuya kwa niaba ya Mkuu ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi