loader
Picha

Halmashauri zitumie vizuri misaada ya Japan

Msaada huo utasaidia upatikanaji wa huduma ya maji katika Sekondari ya Kigwe wilayani Bahi Mkoa wa Dodoma ambapo Shilingi mil 240 zimetolewa kuimarisha ugavi wa maji pia soko la samaki la Nyakarilo ambalo litakarabatiwa na kuwa la kisasa zaidi na hivyo kukuza biashara na kuendeleza ajira.

Sekta ya elimu ndiyo imeonekana kunufaika zaidi ambapo Shilingi mil 173 zimetolewa kwa ujenzi wa Hosteli na kununua samani Sekondari ya Manispaa Moshi huku Shilingi mil 219 zikitolewa kupanua miundombinu Shule ya Msingi Kigoma huku wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya ikisaidiwa Shilingi mil 135 kwa ajili ya ujenzi wa hosteli za wanafunzi.

Binafsi ninaona kuwa serikali hiyo ya Japan imefanya vyema na kuwa ni rafiki wa kweli anayetaka kusaidia kubadilisha maisha ya wananchi.

Hata hivyo, ninachotaka kusema hapa, misaada hiyo isiyokuwa na masharti iwe ni chachu ya mafanikio kwenye maeneo lengwa ambapo wakurugenzi wa halmashauri wanapaswa kuhakikisha kuwa fedha zinaenda kusaidia walengwa.

Ninachowaomba wakurugenzi kutokea halmashauri zilizopelekewa misaada hiyo kuhakikisha kwamba wanasimamia utekelezwaji wa miradi hiyo kwa umakini.

Nasema hivyo kwa kuwa miradi iliyokusudiwa ikitekelezwa itasaidia sana kuleta mabadiliko katika jamii husika. Natoa wito kwa wadau wengine kujitokeza na kutoa misaada ya moja kwa moja inayolenga kubadilisha maisha ya watu kama ilivyofanya serikali ya Japan kupitia ubalozi wake hapa nchini.

Licha ya misaada hiyo ya kipekee ningependa kuisihi Japan kusaidia pia sekta binafsi ili kuwasaidia wananchi kujiimarisha zaidi kimaisha. Kwa kuisaidia sekta binafsi itakuwa imeisaidia Tanzania kutimiza lengo lake la kuwa nchi ya viwanda ifikapo 2025.

MSIMU wa sikukuu za mwisho wa mwaka umewadia. Siku ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi