loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hanspoppe ataka udhamini wa Azam uangaliwe upya

Akizungumza Dar es Salaam jana Hanspoppe alisema fedha wanazopewa Sh milioni 100 kama udhamini kwa timu za Ligi Kuu bado hazitoshi na kwamba klabu ndizo zinazonyonywa kwa vile wanaporusha matangazo ya Ligi Kuu moja kwa moja ‘live’ mapato yao ya mlangoni hupungua kwani mashabiki wengi hubaki kuangalia kwenye runinga badala ya kwenda uwanjani.

“Azam walisababisha mapato yetu ya mlangoni kushuka msimu uliopita kwa sababu walikuwa wakirusha moja kwa moja mechi zetu hivyo, kati ya mashabiki 10 waliotakiwa kuingia uwanjani watano ndio huingia na wengine wakibaki kuangalia kwenye runinga,” alisema.

Kauli ya Hanspoppe ni kama anaunga mkono uamuzi wa Yanga ambayo toka awali uongozi wake uligoma kusaini mkataba wa ufadhili huo ukisema thamani ya fedha hizo ni ndogo kulinganisha na hadhi ya klabu yao.

Hanspoppe alisema wanachokosea Azam ni kuonesha matangazo siku ileile ya mechi inayochezwa badala ya kurekodi na kuonesha siku inayofuata kama vifanyavyo baadhi ya vituo vya runinga vya kimataifa.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Hanspoppe imechelewa kwani Simba ni miongoni mwa klabu zilizochukua mgawo wa awali wa Sh milioni 25 kutoka kwa Azam kama maandalizi ya Ligi Kuu.

Azam ilitoa Sh milioni 462 ambapo kila timu ilipata Sh milioni 25 kama mgawo wa awali, itatoa fedha hizo kwa awamu nne.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania Silas Mwakibinga alisema timu zote za Ligi Kuu isipokuwa Yanga zilishaingiziwa kwenye akaunti zao mgawo huo.

KLABU ya Simba  imetambulisha  mashindano mapya ya Super  Cup, ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi