loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

HAYA NDIYO MAISHA: Usiangalie fulani atasema nini, anza kutimiza ndoto yako sasa

Inawezekana tangu umekuwa ukiambiwa kwamba huwezi, ukijaribu kitu unaambiwa acha utaharibu, darasani kila mtu anakuona huwezi hata ukinyoosha mkono kujibu swali mwalimu hakuangalii na akikuchagua unajikuta kwa hofu unajibu huku unatetemeka matokeo yake unaishia kuchekwa na darasa zima.

Hali hiyo ndio inazidi kukufanya ushindwe kujiamini kabisa, matokeo yake hata unapokuwa na kujikuta uko ofisini linapokuja suala la kuzungumza ama kuchangia jambo unajikuta unashindwa hata kutoa hoja yoyote au changamoto, na hali hiyo inakufanya unakubali tu kila unachoambiwa hata kama unaona hakifai, lakini kwa sababu ya kutokujiamini unakubali tu.

Hii ni roho ambayo inatembea sana ama kwa kujua au kwa kutokujua. Kwa sababu ya roho hiyo kujidharau na kutojiamini hata ukisema uwaze mambo makubwa nafsi yako inakucheka kuwa huwezi, kwa sababu katika ulimwengu wa roho inaonekana hali hiyo.

Unaweza ukakuta ndani ya nafsi yako kuna sauti kabisa inakunong’oneza ikikuambia huna uwezo wa kulifanya hili au huna uwezo wa kulifanya lile, usithubutu kufanya, utashindwa na watakucheka.

Matokeo yake unaweza ukawa na kazi kutaka kufanya kwa sababu hujiamini unahofia huenda ukiifanya utaharibu, au unaweza ukawa na wazo zuri la kutaka kuanzisha kitu lakini unakuta kuna nafsi ovu ya kutojiamini inakufanya uone huwezi kuanzisha kitu, kukisimamia na kukifanikisha.

Nataka leo uamini kabisa kuwa kila unalofikiria kufanya au kile unachotamani kukifanya una uwezo kabisa wa kuchukua hatua na kukifanya bila woga na ukafanikiwa, kinyume na ile roho ya kujidharau na kutojiamini.

Hebu chukua hatua leo, jaribu kukaa sehemu peke yako, chukua kalamu na karatasi au daftari na kisha andika tabia chanya ambazo unajua unazo.

Hiyo ni hatua ya kwanza ya kujiamini na kuacha kujidharau, andika kwa ujasiri bila kuangalia watu wanakusemaje au wamekuwa wakikusemaje, unachotakiwa hapa ni kuongea na moyo wako.

Jichunguze taratibu na andika tabia zote ambazo unaamini unazo bila kujiwekea mashaka ama kuanza kujichuja mwenyewe, kama ndani ya nafsi na ufahamu wako unaamini ni tabia chanya ulizonazo zinakili katika kitabu au karatasi hiyo.

Utakapomaliza kuziorodhesha anza kuzitafakari, ziweke kwenye akili, moyo na nafsi yako na ujitamkie kwa kumaanisha kuwa hizo ni tabia zako njema na chanya ambazo unaamini zinaweza kukufanya uchukue hatua ya kila unachoamini unaweza kukifanya au kukianzisha.

Kama unaweza bandika katika kioo chako au kwenye ukuta, sehemu ambayo mara kwa mara lazima ukatishe ili kila unapokuwa unajiandaa kutaka kutoka au ukipita unazisoma na kuzikumbuka.

Hatua hii itakusaidia kukujengea msingi wa kujiamini na ujasiri wa kuchukua hatua ya kila unachofikiria, kuamini na kutamani kukifanya bila woga au kuangalia watu wengine watakuambia nini?

Kwa sababu tayari umejiaminisha unaweza kukifanya, hata ukatishwe tamaa kisa gani unaweza. Kumbuka siku zote usiwe adui wa nafsi yako mwenyewe.

Kama nafsi, roho, ufahamu, akili na matamanio yako yanakuaminisha unaweza kulifanya jambo fulani amini unaweza.

Usingalie fulani atasema nini au watakucheka, geuza kibao kuwa wale wanaokucheka na kukudharau ndio hawawezi na wewe unaweza, hapo utakuwa umeondokana na roho ya kusitasita kuchukua hatua na kutimiza ndoto zako.

Waziri Mkuu Mstaafu, ...

foto
Mwandishi: Angela Semaya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi