loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Heko Waziri Mkuu kutoa motisha kwa halmashauri

Motisha huu ambao mwenyewe alisema umelenga kuhakikisha halmashauri hizo zinamalizia mambo muhimu, ikiwemo barabara, inatolewa katika kipindi muafaka kabisa cha taifa kuthamini juhudi binafsi na za pamoja za kuleta maendeleo katika halmashauiri zetu.

Ni dhahiri wakati huu ambapo serikali inapeleka madaraka zaidi katika halmashauri pamoja na mafungu ya maendeleo, kitendo cha kutoa motisha ni dalili wazi za kushawishi wengine kufanya kazi kwa bidii ili kupata zawadi za utumishi mwema.

Pamoja na tunzo hizo, tungelipenda kurejea mwito wa Waziri Mkuu akifungua mkutano wa tatu wa wadau wa Mfuko wa Barabara za Mamlaka za Serikali za Mitaa wa Mwaka wa Fedha 2014/15 wa viongozi wa halmashauri kuwajibika katika kazi zao na kuwa makini.

Tunasema hayo kwa kuwa tunaamini kama alivyoamini Waziri Mkuu kuwa sekretarieti zisipokuwa makini kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, baadhi ya halmashauri zinaweza kuendelea kupata hati chafu kutokana na wajanja wachache kula fedha za Serikali.

Hivyo tunaposifu Halmashauri za Wilaya ya Arusha, Longido, Karatu , Chato, Mbogwe na Nyang'hwale zilizopo Mkoa wa Geita na Halmashauri ya Lushoto, Handeni, Tanga na Mbeya kwa kufanya vyema kiasi cha kupewa tunzo ni vyema kukawa na mikakati ya kukagua miradi ya halmashauri na kudhibiti mchwa wanaokula mitaji ya uongozi.

Ni vyema katika hilo kuhakikisha uongozi unashikamana na kushirikiana ili kuweza kujiondoa katika ubadhirifu kwa kusimamiana na kushauriana bila kulalamika kuingiliana kimajukumu.

Na kwa kufanya hivyo pasi shaka wakurugenzi watajiepusha na tabia ya kuteua wazabuni kwa upendeleo na kuhakikisha wale wanaofanikiwa ni wenye uwezo na watakaoweza kuendesha miradi na hatimaye halmashauri mbalimbali kufanya kazi kwa namna inavyotakiwa.

Kwa kuwa maendeleo ni yetu na wasimamizi ni wakurugenzi tunatoa mwito kwa wakurugenzi na watendaji wengine kuhakikisha kwamba kauli za Waziri Mkuu zinajishajihisha kwa wananchi ili mfumo mzima uweze kukidhi maendeleo.

RIPOTI ya 15 kuhusu uchumi wa Tanzania ya ...

foto
Mwandishi: mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi