loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hongera mshindi wetu wa Insha ya SADC

Pongezi hizo pia ziende kwa walimu wake na wazazi kwa kumlea na kumwongoza vizuri hadi kufikia ushindi huo, ambao jumla ya wanafunzi 39 kutoka nchi 13 za jumuiya hiyo, walikuwa wanawania.

Katika habari iliyochapishwa na gazeti hili jana lenye kichwa cha habari ‘Mtoto wa Kitanzania ashinda insha SADC’, tulieleza pia kwamba huyo ni mtoto wa pili kutoka shule za kawaida za sekondari za kata, kushinda tuzo ya kimataifa katika uandishi wa insha.

Mtoto huyo ametanguliwa na mwenzake wa shule ya sekondari ya kata ya Tushikamane ya mjini Morogoro, Peter Kilave aliyekuwa kidato cha tatu, kushinda Tuzo ya Insha Bora katika Jumuiya ya Afrikia Mashariki (EAC) mwaka jana.

Hakuna ubishi kwamba tuna kila sababu ya kujivunia ushindi wa mtoto wetu Neema ambaye kama alivyo mwenzake Peter, wametoka katika shule za sekondari za kata.

Katika hali ya kawaida, pengine tungefikiri kwamba washindi hao wote wawili, wangetoka kwenye shule zile ambazo wengi tunazifahamu kwa majina makubwa tu, kwamba ndizo zinazoongoza katika kutoa matokeo bora, kutokana na aina ya shule zenyewe, uzoefu, ukongwe na walimu wenye ubora wa hali ya juu.

Lakini shule wanazotoka washindi wetu hao wawili ni za kawaida na hii inadhihirisha kwamba tukijipanga vizuri, kuwapatia mazingira bora, walimu wa kutosha wenye ubora, maabara na malezi stahiki, watoto wetu wanaweza kufanya vizuri kama watoto wengine wanaosoma katika shule zenye sifa, tulizoanisha hapo awali.

Ushindi huo uwe chachu ya kuziimarisha shule zetu za kata, kwa kuzipatia walimu bora, vifaa, vitabu vya kutosha na maabara na kuboresha mazingira na maslahi ya walimu wetu ili kupata matokeo mengi mazuri ya watoto, watakaoweza kuendesha nchi yetu kikamilifu katika siku za usoni.

Tunapenda kuwakumbusha wazazi na wananchi kuwa matokeo haya, siyo ajali bali ni maandalizi ya kutosha na watoto wetu kufahamu vyema nafasi yao kama wanafunzi kwa kusoma na kuzingatia kwa makini, waliyofundishwa na walimu pamoja na wazazi wao na hatimaye kutuletea ushindi huu, ambao kila mmoja wetu mwenye akili timamu anaufurahia.

Itakuwa furaha iliyoje, kama tuwapata watoto wa Kitanzania wengine zaidi kama walivyo Peter na Neema? Hili linawezekana kwa kuimarisha miundo mbinu na kujizatiti kwa kuboresha maslahi ya walimu wetu na mazingira ya shule. Tusikubali kushindwa, kwa sababu anayekubali kushindwa, siyo mshindani.

RIPOTI ya 15 kuhusu uchumi wa Tanzania ya ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi