loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Hospitali kutumia bil. 6/- za NHIF kwa miundombinu

Fedha hizo ni mkopo kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Mhandisi Mwandamizi kutoka NHIF, Simon Seleman alisema hayo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, wanaohudhuria mkutano wa siku mbili kupitia mafanikio na changamoto mbalimbali za utoaji huduma kupitia mfuko huo.

Waandishi hao walifanya ziara katika hospitali hiyo ya mkoa, kuona hali ya utekelezaji wa mradi huo.

Mhandisi huyo alisema ujenzi huo unahusisha ujenzi wa jengo la kulaza wagonjwa, litakalokuwa na uwezo wa kuchukua wagonjwa 30 kwa wakati mmoja.

Sambamba na hilo, Selemani alisema pia ujenzi huo unahusisha ujenzi wa vyumba vya kutoa huduma mbalimbali za uchunguzi wa magonjwa na wodi maalumu za kulaza viongozi wa juu wa serikali.

Alieleza ujenzi huo unaenda sambamba na uwekezaji wa vifaa tiba na jengo hilo linatarajiwa kuanza kutumika mwezi Februari mwaka ujao.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya mkoa Dodoma, Dk Ezekiel Mpya alisema ujenzi huo utawezesha kuleta maboresho na mapinduzi makubwa katika utoaji huduma za afya kwenye hospitali hiyo.

Alisema kwamba ujenzi huo, utaondoa msongamano uliokuwepo katika kliniki iliyokuwa ikitumika awali na wagonjwa wanaohudumiwa kwa kutumia bima ya afya.

Alisema kwa sasa kliniki hiyo inahudumia kati ya wagonjwa 40 hadi 50 wanaotumia bima ya afya na kwamba kufanyika kwa maboresho hayo, kutawezesha kuongeza maradufu idadi ya watu ambao watapata huduma katika hospitali hiyo.

Sambamba na ujenzi huo wa jengo maalum la utoaji huduma kupitia bima ya afya, Mganga huyo wa mkoa Dodoma alisema pia hospitali hiyo imeingia mkataba na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, ambapo mkataba huo utaiwezesha hospitali hiyo kununua vifaatiba vyenye thamani ya Sh milioni 570.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo ya waandishi hao wa habari, Ofisa Mawasiliano mwandamizi wa NHIF, Luhende Singu alisema kwa mwaka huu wa fedha mfuko huo unatarajia kutumia Sh bilioni 10 kutoa mikopo kwa hospitali na vituo vya utoaji huduma ya afya ili kuboresha maeneo yao ya utoaji huduma.

Mkuu wa wilaya na Arumeru Jerry ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi