loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hoteli ya Blue Pearl yatupiwa virago

Tukio la hoteli hiyo kutupiwa vyombo vyake nje ilifanywa jana na kampuni ya udalali ya Majembe baada ya kuamriwa na mmiliki wa jengo hilo ambayo ni Kampuni ya Ubungo Plaza Investment.

Hali hiyo ilizua tafrani kutokana na ukweli kwamba hoteli hiyo haikupewa taarifa na wakati Majembe wanafika hotelini hapo, shughuli mbalimbali za hoteli zilikuwa zinaendelea ikiwemo mikutano mbalimbali.

Wafanyakazi wa Majembe chini ya mkuu wao, Seth Mwamoto walifika hotelini hapo wakiwa kwenye lori lenye namba za usajili T 389 AGG na kuanza kuondoa samani mbalimbali ndani ya hoteli hiyo na kuvirundika kwenye gari hilo, jambo ambalo liliushtua uongozi wa hoteli.

Wamiliki wa hoteli hiyo walikimbia kwenda kulipa sehemu dola za Marekani 120,000 kati ya deni la dola za Marekani 380,000.

Kutokana na hatua hiyo ya kuondoa vyombo, shughuli zote za hoteli hiyo zilisimama na mikutano iliyokuwa inaendelea ilifanyika chini ya uangalizi wa karibu wa maofisa wa Majembe ambao walikuwa wanasubiri imalizike waweze kusoma samani zilizoko kwenye kumbi za hoteli hiyo.

Hadi gazeti hili linaondoka eneo hilo la tukio, mazungumzo yalikuwa yanaendelea lakini hata hivyo, sharti la mwenye jengo ni kwa mpangaji kulipa fedha hizo jana na la sivyo agizo la kuendelea kutoa vyombo lingeendelea.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Shadrack Sagati

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi