loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hukumu kesi Bunge Maalum Septemba 22

TLS imewasilisha ombi hilo kwa lengo la kutaka kibali cha Mahakama ili wafungue kesi kupinga mwenendo wa Bunge la Katiba pia itamke kuwa mwenendo wa bunge hilo ni batili.

Wakiwasilisha hoja zao jana, Wakili wa TLS Mpare Mpoki aliiomba Mahakama iwape kibali cha kufungua kesi hiyo kwa kuwa wana hoja za msingi ambazo Mahakama inatakiwa iziangalie.

Hata hivyo, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju akisaidiwa na Wakili wa Serikali Mkuu Gabriel Malata, waliomba Mahakama isitoe kibali kwa kuwa ombi hilo halina msingi kisheria.

Aidha, walidai Mahakama haina mamlaka ya kutoa kibali hicho kwa kuwa ombi la TLS linahusisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar lakini sheria waliyoitumia kuwasilisha ombi hilo inatumika Tanzania bara pekee.

Aliongeza kuwa kifungu cha sheria ya mabadiliko ya Katiba wanachoomba kirekebishwe kinazihusu pande zote mbili na hana uhakika kama wanasheria wa Zanzibar wamehusishwa, hivyo Mahakama haiwezi kutoa uamuzi unaozihusu pande zote mbili wakati upande mmoja haupo.

Katika kesi wanayotaka kufungua TLS, wanaiomba Mahakama itoe tafsiri ya mamlaka ya bunge hilo kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba namba 8 ya mwaka 2011 na namba 2 ya mwaka 2012 Sura ya 83.

Aidha, wataomba Mahakama itoe amri ya zuio la vikao vya bunge hilo pia imuamuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wawasilishe bungeni muswada wa marekebisho ya sheria hiyo.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali ...

foto
Mwandishi: Flora Mwakasala

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi