loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Humoud wa Simba aenda Sofapaka

Hamoud ambaye msimu uliopita alikuwamo katika kikosi cha Simba kilichoshika nafasi ya nne, anaombewa Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) ili akacheze soka ya kulipwa nchini humo.

Kiungo huyo hakuwa na msimu mzuri Simba kwani hakuwa na namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza chini ya makocha Abdallah Kibadeni na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na baadaye Zdravko Logarusic na msaidizi wake, Selemani Matola.

Amewahi kuzichezea pia timu za Mtibwa Sugar ya Morogoro na Azam FC ya Chamazi, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Hamoud ni miongoni mwa wachezaji watano walioombewa ITC ili wacheze mpira wa miguu nchini na nje ya Tanzania.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura, wachezaji wengine ni Crispin Odulla (Coastal Union) na Haji Ugando (Mbagala Market FC) wameombewa ITC na Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) ili wakacheze nchini humo katika klabu za Bandari FC na Nakuru All Stars.

Odulla ni raia wa Kenya ambaye awali alikuwa akichezea Bandari kabla ya kujiunga na timu hiyo ya Tanga msimu uliomalizika, ambako mwishoni wachezaji wengi nyota waliwekwa kando.

Vilevile, TFF imemuombea ITC mchezaji Ismaila Diarra kutoka Mali ili ajiunge na Azam FC. “TFF inafanyia kazi maombi hayo, na mara taratibu zote zitakapokamilika itatoa ITC hizo kwa wachezaji wanaokwenda nje ya Tanzania,” alisema Wambura.

Katika hatua nyingine, Timu ya taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) inaendelea vizuri na mazoezi kujiandaa kwa mechi ya mashindano dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos).

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili itachezwa Ijumaa ya Julai 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Hababuu Ali Omari ameshafanya mchujo wa awali wa wachezaji wa timu hiyo kutoka 39 na kubaki na 31. Timu hiyo imepiga kambi kwenye Hosteli ya TFF iliyopo Uwanja wa Karume.

BAADA ya kumtwanga Mkenya, Daniel Wanyonyi, bondia Mtanzania, ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi