loader
Picha

Ilala Academy, Champion zamaliza ARS kwa kishindo

Mabao hayo yalifungwa na Rashid Mohamed dakika ya 19, Maisala Adam dakika ya 44 na Edward Jonas dakika ya 45.

Katika mchezo mwingine wa funga dimba uliopigwa uwanjani hapo, mshambuliaji machachari wa Champion ya Kinondoni, Abubakar Mussa alifunga mabao matatu na kuiwezesha timu yake kuifunga Chipukizi 3-2.

Mchezo huo wa kusisimua ulishuhudiwa na mashabiki wengi waliokuja kushangilia timu zao. Ilikuwa ni Chipukizi walioanza kupata bao la kwanza lililofungwa na Ally Amin.

Bao hilo lilipokelewa kwa shangwe na mashabiki wa Chipukizi ambao walikuwa wakishangilia timu yao tangu mwanzo hadi mwisho.

Hata hivyo, furaha yao iliingia dosari baada ya Mussa kufanya kazi ya ziada na kusawazisha kwa shuti kali ambalo kipa wa Chipukizi alishindwa kulizuia.

Mussa aliyekuwa mwiba mkali kwa Chipukizi, alifunga bao la pili dakika ya 34 alipoachia shuti la chini chini na kuandika bao la pili. Hadi mapumziko, washindi walikuwa wanaongoza mabao 2-1.

Baada ya mapumziko, Champion waliingia kwa ari mpya na Mussa kufunga bao la tatu kabla Chipukizi hawajafunga bao la pili kwa Mohammed Abdallah.

MABINGWA wa kihistoria Yanga leo wanashuka dimbani kuikabili Tanzania Prisons ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi