Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu wa Asasi hiyo David Msuya alisema, wajasiriamali hao ambao ni watumishi wenye ajira wameweza kupata mikopo hiyo kwa awamu mbalimbali.
Alisema, wajasiriamali walionufaika na mkopo huo ni kutoka Mpwapwa mkoani Dodoma, Mbezi na Manzese jijini Dar es Salaam, Pwani, Kilombero na Mbuyuni mkoani Morogoro.
Aidha aliwataka wajasiriamali kuhakikisha wanatambua sheria za mikopo na kuzitimiza ili waweze kupata mkopo na kuacha tabia ya kulalamika na kudai kuwa asasi mbalimbali zinatoa mikopo kwa njia ya rushwa au kwa kujuana jambo ambalo si la kweli.
Hata hivyo Msuya alisema kuwa wamekuwa wakitoa mkopo kwa wajasiriamali mbalimbali nchini kupitia mradi wa boresha makazi ya mtumishi unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Ujerumani (Global It) ili kuwawezesha kuboresha biashara zao na hatimaye kuboresha makazi yao.