loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

IPTL kupeleka megawati 2000 za umeme Kenya

Hatua hiyo inatokana na kukamilika kwa mazungumzo baina ya kampuni hiyo na Serikali ya Kenya.

Katika kuthibitisha utekelezaji wa mradi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Petroli wa Kenya, Joseph Njoroge amesaini barua ya makubaliano Agosti 19, mwaka huu kwenda kwa Mwenyekiti Mtendaji wa Pan African Power (PAP), Harbinder Sing Sethi.

Taarifa zaidi kuhusiana na barua hiyo, yenye kumbukumbu namba ME&D/CONF/3/2/73A zinabainisha kuwa pande zote tatu yaani PAP, Tanzania na Kenya zikutane haraka kuona ni namna gani uzalishaji huo utaanza haraka iwezekanavyo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu na Mwanasheria Mkuu wa PAP, Joseph Mwakandege alisema kampuni yao inamejizatiti kutekeleza miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi badala ya kuendeleza malumbano ya kisiasa ambayo hayaleti tija kwa taifa.

“Tunafurahi kuwa tunazidi kuaminiwa na serikali mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. Hii inadhihirisha ufanisi na ueledi wetu katika tasnia nzima ya nishati,” alisema.

Pia amezishauri kampuni nyingine za kuzalisha umeme kuelekeza utaalamu katika kuwatumikia wananchi badala ya kupigana vijembe ambavyo huzaa chuki na kudhoofisha kasi ya maendeleo ya wananchi.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi