loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

IPTL kushusha bei ya umeme

Katibu na Mshauri wa sheria IPTL/PAP, Joseph Makandege alisema hayo jana kupitia taarifa kwa vyombo vya habari ambayo pamoja na kuelezea masuala mbalimbali ya kampuni, alikuwa akimjibu Mbunge wa Kigoma Kusini , David Kafulila kuhusu shutuma zake dhidi yao.

Makandege alisema licha ya kuwapo maadui wa kibiashara wakiwemo baadhi ya wanasiasa wanaotumiwa, watahakikisha wanaendelea na uzalishaji.

“Tunawahakikishia Watanzania tutaendelea kuzalisha na kuwauzia umeme wa uhakika na kwa bei nafuu na mchakato wetu wa kushusha bei ya umeme kutoka 450 ya sasa kwa uniti mpaka sh 80 uko mbioni kukamilika.”

Alisisitiza kwamba lengo la kufanya hivyo ni kuwezesha Watanzania kufurahia na kunufaika na huduma ya umeme ili wachangie maendeleo yao.

Hata hivyo alisema wapo wapinzani wao wa kibiashara ambao hawapendi Watanzania wafaidi matunda ya kampuni hiyo.

Katika taarifa hiyo, Makandege alimtaja mbunge huyo kuwa amekuwa akilazimisha masuala yasiyo sahihi juu ya kampuni yaaminiwe na umma.

Kwa mujibu wa mwanasheria huyo, inafahamika wazi kwamba IPTL ni mali ya PAP, baada ya VIP na Mechmar kuuza hisa zao kwa PAP ingawa baadhi ya wanasiasa wanapotosha ukweli.

“Na hili jambo sio siri na limeripotiwa katika vyombo vyote vya habari Tanzania,” alisisitiza.

Kampuni hiyo ya kufua umeme imemshutumu mbunge huyo kwa kile alichosema anahamasisha mijadala kiasi cha kumhusisha Waziri Mkuu, Baraza la Mawaziri juu ya suala la fedha za Escrow akifahamu ni jambo la kisheria na si la kisiasa.

“Yalikuwa malipo halali kwa IPTL/PAP na huo ndio ukweli na utaendelea kuwa hivyo, na ningemshauri Kafulila ajifunze nini maana ya Escrow hata kwa njia ya mtandao ili siku nyingine asiendelee kulishwa bila kujua ukweli wa ndani,” alisema.

Hivi karibuni katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kafulila alitishia kwamba iwapo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) hazitatoa ripoti kuhusu kile anachodai ni ufisadi wa Sh bilioni 400, Bunge la Novemba halitakalika.

KAMPUNI ya Vodacom Tanzania imetangaza ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi