loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

IPTL yashusha bei ya umeme

Katibu na Mshauri wa Sheria PAP/IPTL, Joseph Makandege alisema kwa sasa mitambo yao ya kuzalisha umeme inatumia mafuta mazito, ambayo yana gharama kubwa katika uzalishaji umeme.

Alisema uzalishaji umeme kwa kutumia mafuta hayo ni gharama kubwa, hasa katika usafirishaji na hivyo kusababisha wauze umeme wanaozalisha na kuuzia Tanesco kwa gharama kubwa.

“Tutakapoanza kutumia nishati mbadala ya gesi, kila kitu kitakwenda vizuri na gharama za umeme tunayouzia Tanesco zitapungua kwa kiasi kikubwa.

“Tunaamini hadi mwakani matumizi ya nishati ya gesi yatakuwa tayari, hivyo tutanza kutumia gesi katika uzalishaji umeme na lazima bei yetu ya umeme itashuka kwa Tanesco.

Makandege alisema PAP/IPTL inawataka Watanzania wawe wavumilivu wakati ipo katika mchakato wa kupunguza gharama za mauzo ya umeme kwa Shirika la Umeme nchini (TANESCO).

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi