loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Isakalilo, Ilala nguvu sawa la Nne Iringa

Ligi hiyo inayofadhiliwa na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalebela, ulishuhudia timu hizo zikioneshana ufundi wa kutandaza soka na kufanya matokeo kuwa sare.

Isakalilo FC ndio walioanza kuzifumania nyavu za Ilala FC katika dakika ya 38 lililofungwa na Pingaki Hussein bao ambalo lilidumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko na kufanya mchezo kuwa wa kushambuliana kwa zamu na dakika ya 76 Ilala FC, ilifanikiwa kusawazilisha bao lililofungwa na Hamis Said.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Iringa, Katibu wa Chama cha Soka Manispaa ya Iringa (IMFA), Rashid Shungu alisema mchezo ulikuwa mzuri na wenye ushindani.

“Mchezo ulikuwa mzuri na kila timu ilionyesha kuhitaji kuondoka na pointi tatu lakini kutokana na ushindani waligawana pointi moja moja,” alisema Shungu.

Ligi hii ipo katika hatua ya sita bora na ilianza kutimua vumbi Februari mosi na inatarajiwa kumalizika Machi 22, mwaka huu kwani inachezwa nyumbani na ugenini. Leo Mtwivila FC wataikaribisha Mtwa FC katika mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Samora.

Klabu ya Liverpool na Manchester United zipo vitani kumuwinda ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi