loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jaji kiongozi akemea mavazi yasiyo ya heshima

Pia amewataka mahakimu na majaji nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ikiwa ni pamoja na kuachana na urasimu usio wa lazima katika utoaji wa dhamana kwa watuhumiwa ili kupunguza malalamiko yanayotolewa na wananchi dhidi ya mahakama.

Ametoa wito huo mkoani hapa wakati akizungumza na watumishi wa idara ya Mahakama ambapo yupo mkoani hapa kwa ziara ya kikazi kwenye mikoa ya Mara, Geita na Mwanza.

Jundu ametumia nafasi hiyo ya kuzungumza na wafanyakazi wa Mahakama kuu kanda ya Mwanza na kuwakumbusha umuhimu wa kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu ili kuwa mfano wa kuigwa katika jamii.

Akizungumzia maadili kwa maofisa wa mahakama aliwataka kuzingatia mambo mbalimbali ikiwemo ya kuepukana na rushwa, kiburi na ubabe, ulevi, kuchelewa kazini, kuepuka uanaharakati ama shughuli za kisiasa.

Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili ...

foto
Mwandishi: Garce Chilongola, Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi