loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jaji Mihayo Rais mpya MCT

Baraza hilo lililoketi mjini Bagamoyo mkoani Pwani, pia limemchagua Hassan Abdallah Mitawi, Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) kuwa Makamu wa Rais kwa baraza hilo.

Rais mpya wa MCT, Jaji Mihayo amechukua nafasi hiyo kutoka kwa Jaji mstaafu Robert Kisanga, ambaye muda wake wa kutumikia baraza hilo kikatiba umemalizika.

Akitangaza matokeo hayo, Mwenyekiti wa Uchaguzi huo, Jane Mihanji alisema uchaguzi huo umewarejesha kwenye Bodi hiyo ya MCT, Badra Masoud ambaye ni Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini na Rose Haji, ambaye ni mwandishi mkongwe, kuendelea na wadhifa wao.

Kulingana na Katiba ya MCT, wajumbe wawili wa Bodi hiyo wanaomaaliza muda wao, wanaruhusiwa kuchaguliwa tena, kuendelea na wadhifa huo kwa kipindi kingine.

Wajumbe wapya waliochaguliwa kujiunga na bodi hiyo kutoka kundi la waandishi wa habari ni Tuma Abdallah, ambaye ni Mhariri wa gazeti la Daily News na Wallace Maugo, ambaye ni Mhariri wa gazeti la The Guardian.

Kutoka kwenye kundi la jamii, waliochaguliwa kwenye bodi hiyo ni Profesa Bernadetha Killian, ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa cha Chuo Kikuu cha Dar es Saalam na Ali Mfuruki ambaye ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Wananchi Group yenye bidhaa za ZUKU na Jaji mstaafu Juston Mlay.

RAIS John Pombe Magufuli amewataka wabunge ...

foto
Mwandishi: Nicodemus Ikonko, Bagamoyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi