loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jambazi raia wa Kenya auawa Tarime

Mbali ya mkazi huyo wa Nchoke, mwingine anatajwa kuwa ni jambazi raia wa Kenya aliyekuwa amekimbilia nchini baada ya kufanya uhalifu nchini mwake, lakini katika mapigano hayo alipigwa mshale ubavuni na baada ya kuanguka alikatwa mapanga hadi mauti yalipomfika.

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi Tarime/Rorya, Lazaro Mambosasa ambaye alisema, ”Tukio hilo lilitokea Septemba 17, mwaka huu saa 12 jioni katika Kitongoji cha Nchoke Kijiji cha Kubiterere, Kata ya Mwema.

Kamanda huyo alisema watu watatu waliokuwa na bunduki mbili aina ya SMG na mapanga walishambuliwa baada ya kufanya ujambazi kwa mfanyabiashara aitwaye Muungwana Ghati Rwaya ambapo wananchi wenye hasira waliamua kupambana nao.

“Wakapiga kelele kuomba msaada wa vijiji vya jirani na ndipo wanavijiji wakiwa na silaha za jadi wakajitokeza kupambana nao. Hapo mwenzao mmoja akauawa baada ya kupigwa risasi ya mgongoni.

“Kuona hivyo, kasi ya mapambano ikawa kubwa, risasi zikipigwa hovyo na wananchi wakijibu kwa kurusha mishale na mawe na kufanikiwa kumpiga mshale mmoja wao aliyeanguka, lakini kabla ya kufika chini alimpa bunduki mwenzake aendelee na mapambano. Alipoanguka walimkata kwa mapanga hadi kumuua huku majambazi wengine wakikimbia.”

Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Wilaya Tarime ikisubiri kuchukuliwa na ndugu za marehemu kwa maziko.

WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na ...

foto
Mwandishi: Samson Chacha, Tarime

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi