loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Japan kusaidia ujenzi wa soko la kisasa la samaki

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalumu ya SMZ, Haji Omar Kheir alisema hayo wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi kwa tiketi ya CUF, Saleh Nassor Juma aliyetaka kujua lini Serikali itajenga soko la kisasa ili kuepuka wafanyabiashara wa mnada wa samaki kufanya shughuli zao katika maeneo ambayo sio rasmi.

Alikiri na kusema wapo wafanyabiashara wengi wa samaki wanafanya biashara katika maeneo ya nje, ikiwemo barabarani na sio maeneo rasmi yaliyowekwa.

Alisema zipo sababu nyingi zinazosababisha wafanyabiashara wa samaki kufanya kazi zao katika maeneo ambayo sio rasmi, ikiwemo ufinyu wa sehemu zilizotengwa kwa kazi hiyo.

“Wafanyabiashara wetu wa samaki wanafanya kazi zao katika maeneo ambayo sio rasmi, ikiwemo barabarani na kusababisha usumbufu mkubwa na kuweka mazingira ya uchafu,” alisema.

Aidha alisema baadhi ya wafanyabiashara wanakwepa kufanya kazi zao za kuuza samaki katika maeneo yaliyotengwa kwa kukwepa kutoa kodi iliyowekwa na Manispaa.

Alisema kujengwa kwa soko kubwa la kisasa katika eneo la Malindi kwa kiasi kikubwa kutasaidia na kuwafanya wafayabiashara hao kutambuliwa na kulipa kodi sahihi.

Kheir alisema kilichojitokeza kwa sasa ni kwamba wafanyabiashara wa samaki hulazimika kupambana na askari wa Manispaa kwa sababu ya kufanya kazi zao kinyume na sheria.

Alisema ujenzi wa soko la kisasa la samaki katika eneo la Malindi unatazamiwa kugharimu jumla ya Sh bilioni 14 ambazo zitatolewa na Serikali ya Japan.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi