loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jarida la Wanawake: Idd itumike kusameheana na kudumisha upendo

Idd ni sikukuu inayokuja baada ya kumalizika kwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo Waislamu hufunga kwa siku 29 au 30 bila kula mchana wala kunywa maji.

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni maalumu na unajulikama pia kama mwezi wa Rahma, mwezi wa Baraka, ni mwezi wa kumtii Mwenyezi Mungu, Ramadhani ni mwezi wa Imani, ni mwezi wa Msamaha, ni mwezi ambao ndani yake kuna ‘usiku’ (mmoja) ambao ni bora kuliko miezi 1,000.

Mwezi Mtukufu unatoa nafasi ya kusameheana ili kuondoa visasi, vinyongo, chuki na vikwazo vyote vinavyozuia thawabu kutoka kwa Allah.

Njia pekee ya kuendelea kupata baraka ni kuenzi kazi na upendo wa Mtume Muhammad (S.A.W) ambaye amehimiza Waislamu kuacha dhambi na kuishi katika misingi yenye maadili mema kwa kuzingatia maandiko ya Kuraani Tukufu.

Mawaidha ya dini ya Kiislamu yanaeleza kuwa msamaha huleta maelewamo baina na ndugu, jamaa na marafiki. Hivyo kama una chuki au uhasama na jirani, ndugu, au rafiki yako ni vyema kusamehe ili uweze kusherehekea Idd ukiwa na moyo mkunjufu.

Pia huu ni wakati muafaka kwa wenye ndoa kutathmini mahusiano yao kuboresha upendo na mshikamano na kuweka misingi bora ya kulea watoto ili kuwa na familia bora inayozingatia misingi wa dini ya Kiislamu.

Wanawake waliofikia hatua ya kuvunja urafiki na ushirikiano katika miradi ya maendeleo kutokana na makosa mbalimbali wanapaswa kusameheana, kusahau yaliyopita na kuweka mikakati ya kusonga mbele kwa upendo na mshikamano ili kuondokana na umasikini. Nawatakia heri ya Sikukuu ya Idd el Fitri.

Naamka asubuhi,  sioni kilongalonga, 
Napapasa kitandani,  hamadi hiki hapa,  

foto
Mwandishi: Kaanaeli Kaale

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi