loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jarida la Wanawake: miaka 50 ya Muungano

Muungano huo wa kipekee unastahili pongezi za dhati kwa kuwa umedumisha umoja, mshikamano, amani na utulivu katika taifa hili changa. Watu wenye mapenzi mema naTanzania wanausifia na kupongeza Muungano huo.

Hata hivyo kuna baadhi ya watu wanaotamani kuona Muungano ukisambaratika kwa sababu hawapendi kuona nchi masikini hasa za Kiafrika zikiwa na utawala imara uliojengeka katika msingi wa amani na utulivu.

Wakati Watanzania wanafurahia mafanikio makubwa ya Muungano huo, kuna baadhi ya watu ndani na nje ya nchi wanaokerwa na jinsi Tanzania inavyoweza kudumisha amani na utulivu pamoja na kusaidia nchi nyingine za Afrika kulinda amani.

Baadhi ya watu wanataka kutumia Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba kudhoofisha Muungano huo ambao ni tunu na urithi wa kipekee kwa Taifa la Tanzania.

Kwa kutambua changamoto za Muungano, Watanzania na hasa wanawake wanapaswa kuwa makini kuhusu hila ya kuvunja Muungano kwa kuwa wanawake na watoto ni waathirika wakubwa wa matokeo hafifu ya kisiasa iwe gharama kubwa za kuendesha serikali au machafuko ya kisiasa.

Changamoto iliyopo sasa ni kuulinda Muungano kwa miaka mingine 50 ijayo ili kuepuka kutoa mwanya kwa maadui wanaotaka kuona Watanzania wakisambaratika.

Ili kudumisha muungano huo, wanawake wanapaswa kuweka mikakati thabiti ya kuwarithisha vijana na watoto misingi mizuri ya kuthamini na kupenda Taifa lao ili kudumisha Muungano.

Kwa kuwa umoja ni nguvu, utengano ni dhaifu, Watanzania wanapaswa kukataa sera za kudhoofisha umoja wetu kwa kutumia kisingizio cha aina yoyote ile. Kinachotakiwa ni kuimarisha muundo wa ugawaji wa madaraka katika muundo wa Muungano kwa pande zote mbili.

UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Riadha ...

foto
Mwandishi: Kaanaeli Kaale

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi