loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jarida la Wanawake: Pasaka itumike kusameheana na kudumisha upendo

Kwa kujibu wa Wakristo, Pasaka hutumika kukumbuka mateso na kifo cha Yesu Kristo aliyesulubiwa na kutundikwa msalabani ili kuwaokoa wenye dhambi.

Njia pekee ya kuenzi kazi na upendo wa Yesu Kristo ni kuacha dhambi na kuishi katika misingi yenye maadili mema.

Pasaka inatoa nafasi ya kusamehe ili nawe upate kusamehewa ili kuondoa visasi, vinyongo, chuki na vikwazo vyote vinavyozuia furaha ya kweli kutoka moyoni.

Kwa kuzingatia mafundisho ya Yesu Kristo, ni vyema kutumia Pasaka hii kusamehe wale wote waliokukosea au kukukwaza ili kufungua ukurasa mpya wa maisha yenye furaha, upendo na amani moyoni.

Mafundisho ya dini yanaeleza kuwa msamaha huleta maelewano baina na ndugu, jamaa na marafiki. Msamaha huondoa mzigo wa dhambi kwa waliokosea na waliokosewa, kitendo ambacho kinapunguza maradhi na kuongeza siku za kuishi.

Historia inaonesha kwamba Yesu Kristo alipigwa hata wakati akiwa hai, lakini kazi na mafundisho yake yanaendelea kupata umaarufu karidi miaka inavyosonga mbele. Hivyo Wakristo wanapaswa kutafakari na kurejea kwenye mafundisho ya dini ili kudumisha amani na upendo kwa watu wote.

Kama una chuki au uhasama na jirani, ndugu, au rafiki yako ni vyema kutumia Pasaka hii kusamehe na kufuta uhasama ili nawe uweze kupokea msamaha wa dhambi na baraka za Mungu.

Huu ni wakati mwafaka kwa wenye ndoa kutathmini mahusiano yao kuboresha upendo na mshikamano na kuweka misingi bora ya kulea watoto ili kuwa na familia bora.

Wanawake waliyofikia hatua ya kuvunja urafiki na ushirikiano katika miradi ya maendeleo kutokana na makosa mbalimbali wanapaswa kusameheana, kusahau yaliyopita na kuweka mikakati ya kusonga mbele kwa upendo na mshikamano ili kuondokana na umasikini.

UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Riadha ...

foto
Mwandishi: Kaanaeli Kaale

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi