loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jarida la Wanawake: Serikali ichukue hatua kali dhidi ya vigodoro

 

Kinachosikitisha zaidi ni kwamba baadhi ya wanawake hao hucheza hadharani katika sehemu za wazi tena mchana kweupe na kusababisha watoto wadogo na vijana kushuhudia wanawake wakigalagala chini wakiwa uchi wa mnyama, huku wakiwa wamepanua miguu yao kuonesha waziwazi sehemu zao nyeti.

Kinachosikitisha zaidi, baadhi ya vikundi vya Kigodoro mambo yote hadharani huongozwa na matarumbeta ambayo yanapigwa na wanaume wenye akili zao timamu bila kujali asilimia kubwa ya watazamaji wa mchezo huo ni watoto na vijana.

Katika baadhi ya kanda za ngoma ya Kigodoro mambo yote hadharani zinaonesha wanaume wakielekeza matarumbeta kwa wanawake wanaolala chali kwa lengo la kuonesha kwa wazi zaidi sehemu zao za siri.

Cha kushangaza katika mkanda huo, wasichana wenye umri kati ya miaka 10 hadi 16 wanaonekana wakisikitika na kudhefeheka kiasi cha kutaka kuwafunika wachezaji ila wanawake na wanaume watu wazima wenye umri kati ya miaka 40 na kuendelea wanaonekana kufurahia, huku watoto wadogo zaidi wakishangaa na kuangalia kwa makini mambo ambayo sio ya kawaida kwao.

Hakika utovu huo wa nidhamu ni dhuluma kubwa dhidi ya maadili ya watoto na vijana hasa. Serikali inapaswa kuchukua hatua kali kwa kuanza na viongozi wa mtaa ambao wanaacha madhambi hayo kutendeka waziwazi katika mitaa yao.

NATAKA niwe mkweli kwa nafsi yangu kuwa, hata kama tungekuwa ...

foto
Mwandishi: Kaanaeli Kaale

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi