loader
Picha

JARIDA LA WANAWAKE: Siku hii itumike kupata wanawake imara

Siku hii ambayo kwa mwaka huu imeonekana kuadhimishwa na kuripotiwa kwa wingi katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, ni muhimu ikiwa itatumika vema na siyo kuongeza hofu kwa mtoto wa kike.

Ni dhahiri kuwa mtoto wa kike duniani anakabiliwa na changamoto nyingi ambazo nyingine zinatokana na mitindo ya maisha, mila na desturi, imani na mengineyo ambayo yanamfanya kumdidimiza mtoto huyo.

Mtoto wa kike amekuwa akikabiliwa na matatizo kadha wa kadha ndiyo anapopatikana mwanamke mnyonge asiyejiamini na asiyeweza kufanya maamuzi wakati mwingine kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi kuanzia ngazi ya familia na hata taifa kwa ujumla.

Lakini mtoto wa kike anapojengewa maisha ya kujiamini na kuthamini mchango wake katika jamii, na kulindwa dhidi ya vitendo vya unyanyasaji ndipo tutakapopata wanawake wengi bora na wanaojiamini katika ngazi za maamuzi na kuondoa zana iliyopo kuwa ili mwanamke awepo sehemu anatakiwa kusaidiwa.

Hili linawezekana pale watoto wa kike wanapojengewa misingi hiyo kuanzia ngazi ya familia na hata katika jamii ili kujiona ana thamani kuliko ilivyokuwa awali ambapo alionekana siyo kitu na kuishia kuolewa na kuzaa huku akisubiri maamuzi ya mwanaume.

Dhana hii inatakiwa kuondoka kabisa bila kuathiri mifumo ya asili iliyopo baina ya mtoto wa kike na mwanaume, mfano mzuri ni aliofanya Rais wa Uganda katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike aliamua siku hiyo kumpa nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) mtoto wa kike mwenye miaka 11, Elizabeth Atukunda kushika nafasi hiyo.

Kwa siku hiyo moja, mtoto huyo alikutana na polisi na kuzungumza nao hakika kwa sasa mtoto huyo atakuwa amejijengea jambo katika maisha yake, ikiwa ni pamoja na kujiamini na huko mbele atakuja kuwa mtu mwenye maamuzi makubwa.

Lakini siyo kwa mtoto huyo tu lakini pia wale watoto wa kike walioona, wameona kuheshimika sana na kuaminiwa jambo ambalo linatakiwa kufanyika maeneo mengine kwa kuanzia kwenye familia kwa kuwataka kufanya mambo yatakayowajengea kujiamini.

Lakini katika kumjengea uwezo mtoto wa kike masuala haya yanatakiwa kufanyika siku zote za maisha, bali kuwekewa mkazo katika maadhimisho ya siku hiyo ambayo ni mara moja kwa mwaka.

Ili kuipa uzito ni vema taasisi, mashirika na hata shule za watoto wa kike kwa kushirikiana na serikali kuweka mikakati ya utekelezaji kumjengea mtoto wa kike uwezo na kujiamini na inapofika wakati wa maadhimisho hayo kujipima na kuona hatua zilizopigwa huku kukiwa na malengo mahsusi.

JUZI iliibuka taarifa katika mitandao ya kijamii juu ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko.

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi