loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jarida la Wanawake: Tukileta mzaha homa ya dengue itatuangamiza

Homa ya dengue ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi kinachoenezwa na mbu aina ya Aedes wenye rangi nyeusi na nyeupe. Dalili za ugonjwa huu ni homa ya ghafla, kuumwa kichwa hususani sehemu za macho, maumivu ya viungo na uchovu.

Wakati mwingine dalili za ugonjwa huo zinafanana na ugonjwa wa malaria. Dalili nyingine za ugonjwa wa dengue ni kutokwa na damu kwenye fizi, mdomoni, puani, kwenye macho na pia njia ya haja kubwa na ndogo.

Taarifa za ugonjwa huo zimepokelewa kwa hisia tofauti ambapo wapo watu ambao wamepata hofu kupindukia na wanadhani kuwa ugonjwa huo hauna tiba.

Ukweli ni kwamba ugonjwa huo unatibika ila hauna tiba maalum kama ilivyo kwa ugonjwa wa malaria ambapo kila mgonjwa anaweza kunywa dawa za mseto. Homa ya dengue inatibiwa na dawa mbalimbali kulingana na dalili za mgonjwa.

Pia wapo wanaopuuzia ugonjwa huo na kufanya mzaha, eti kama hawajaogopa virusi vya Ukimwi kwanini waogope virusi vya homa ya dengue. Kuna tofauti kati ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi na virusi vya dengue.

Virusi vya Ukimwi vinaenezwa na watu hasa kupitia ngono isiyo salama wakati virusi vya dengue vinaenezwa na mbu ambaye anaweza kuuma watu wote katika familia.

Endapo watu wa familia hiyo hawatawahi hospitali na kupata tiba sahihi wanaweza kuteketea katika kipindi kifupi. Hivyo ni vyema kuacha woga na mzaha na kuwahi hospitali kupima ili kupata tiba sahihi na kunusuru maisha.

Pia ni vyema kushiriki katika kampeni ya kuangamiza mazalia ya mbu vinginevyo homa ya Dengue inaweza kusababisha janga la kitaifa.

UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Riadha ...

foto
Mwandishi: Kaanaeli Kaale

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi