loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jarida la Wanawake: Wanawake wanapofikia hatua ya kujiingiza kwenye ujambazi

Inadaiwa kuwa mwanamke huyo amekuwa akitumia bunduki aina ya SMG na kushiriki kikamilifu katika matukio ya ujambazi unaoambatana na mauaji ya watu wasio na hatia.

Taarifa za mwanamke huyo zimewashangaza wengi kwa kuwa si kawaida kwa wanawake kushiriki katika ujambazi. Hata hivyo hali ngumu na mabadiliko ya mfumo wa maisha umesababisha baadhi ya wanawake kujiingiza katika vitendo vya uhalifu.

Miaka mitatu iliyopita niliandika katika safu hii juu ya wanawake wakazi wa Mkuranga Mkoa wa Pwani ambao walishawishika kujiunga na vitendo vya ujambazi wa kutumia silaha ili kupata fedha za kutunza familia.

Wanawake hao wenye umri kati ya miaka 19-35 wanasema kuwa kuliko kushuhudia watoto wao wakifa kutokana na ukosefu wa fedha za matibabu ni bora washiriki katika matukio ya ujambazi ili kupata fedha za kuokoa maisha ya watoto wao.

Wanawake hao wasiokuwa na shughuli yoyote ya kuwaingizia kipato wanasema wanahitaji angalau Sh 1,500 kwa siku ili kumudu maisha ambapo mkaa kipimo kimoja Sh 550, maji ndoo moja Sh 150, unga wa mahindi robo kilo 300, matembele fungu moja 200, maji ya kunywa ya watoto watatu angalau glasi moja kwa kila mtoto ni Sh 300.

Mmoja akasema, “hakuna mwanamke anayependa kuiba ila sasa tufanye nini ili watoto waweze kupata angalau mlo mmoja tu tena chakula duni… ugali na matembele bila mafuta?”

Njia pekee ya kuwazuia wanawake kujihusisha na vitendo vya uhalifu ni kuwajengea uwezo wa kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali kwa kuwapatia mafunzo, mitaji na masoko.

Naamka asubuhi,  sioni kilongalonga, 
Napapasa kitandani,  hamadi hiki hapa,  

foto
Mwandishi: Kaanaeli Kaale

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi