loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jihadharini na wizi mpya kwenye daladala

Changamoto hizo ni pamoja na wizi wa waziwazi uliozuka jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya makondakta wa daladala wanawaibia abiria hasa wanawake.

Katika wizi huo, baadhi wasio waaminifu hushirikiana na vijana wengine wanaojifanya makondakta.

Wakati makondakta hao wanapokusanya nauli hurudisha chenji kwa wanaotoa noti za Sh 500 hadi 2000.

Wale wanaotoa noti za Sh 5,000 na 10,000 huambiwa wasubiri hadi chenji itakapopatikana.

Abiria anapofika mwisho wa safari yake na kudai chenji kondakta hudai hajapokea fedha zozote na kuanza kumshambulia abiria kwa matusi. Baadhi ya makondakta huwakashifu abiria kwa madai huwa sura zao zinaonesha kuwa hawana uwezo wa kushika noti ya Sh 5,000 au Sh 10,000 hivyo wasidai kitu ambacho hawajatoa.

Malumbano yanapokuwa makali kondakta hushuka njiani na kisha kupanda kondakta mwingine.

Kondakta mpya anapodaiwa chenji hudai kuwa mwenzie hakumrithisha madeni hivyo kama kuna abiria mwenye malalamiko anapaswa kusubiri hadi siku akikutana na mhusika. Wizi huu mpya umekuwa kero hasa kwa wanawake ambao wanadaiwa kuwa ujira wao mdogo hauwawezeshi kuwa na noti ya Sh 10,000.

Ili kudhibiti wizi huo mamlaka husika zinapaswa kuandaa utaratibu wa kusajili madereva na makondakta wa daladala pamoja na kuwaagiza kuvaa vitambulisho ili waweze kufahamika kwa urahisi mara wanapojihusisha na vitendo vya uhalifu.

Ili kuondokana na kero ya kuibiwa au kupitishwa kituo au usumbufu wa kudai chenji, abiria na hasa wafanyabiashara wanapaswa kuhakikisha wanakuwa na chenji kamili.

UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Riadha ...

foto
Mwandishi: Kanaeli Kaale

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi