loader
Picha

Jitegemee netiboli yatupwa nje Feasssa

Kwa matokeo hayo, Jitegemee sasa ni kama imeaga mashindano baada ya kupokea vipigo vitatu tangu kuanza kwa mashindano hayo.

Washindi walifanya kweli katika robo zote nne, ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 18-0, 34-4 na 48-8. Kocha Mkuu wa timu ya Shule ya Jitegemee Christina Kabamba alisema baada ya mchezo huo, timu yake ilizidiwa.

Alipoulizwa kama wamepoteza matumaini katika mechi mbili zilizobaki, Kabamba alisema hawana matumaini na mechi zilizobaki ni kwa ajili ya kukamilisha ratiba tu.

“Hatuna matumaini ya kufanya vizuri kwani tayari tumeshafungwa mechi tatu na zimebaki mechi mbili tu ambazo hata tukishinda hazitatusaidia lolote,” alisema kocha huyo.

Katika mchezo mwingine wa netiboli jana;, LTP Bujumbura ya Burundi iliibuka na ushindi mnono wa mabao 95-1 dhidi ya Kibuli ya Uganda.

Katika mpira wa wavu, Popatlall ya Tanga ilikiona cha moto baada ya kupokea kichapo cha seti 3-0 kutoka kwa Mwembeladu ya Zanzibar huku Makongo wakitoa kichapo kwa Lord Barden kwa seti 3-2 na Cheptil ya Kenya ikichapwa na St Mary’s ya Uganda kwa seti 3-0.

Kwa upande wa mpira wa kikapu, Rumbeli Sekondari ya Sudan Kusini ilijikuta ikichapwa kwa pointi 63-49 katika mchezo mkali na wa kusisimua.

KLABU ya Simba imeiomba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, ...

foto
Mwandishi: Cosmas Mlekani

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi