loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jitegemee yapata maumivu Feasssa

Katika mchezo huo, Jitegemee ambao ni moja ya timu tatu za netiboli zinazowakilisha taifa, ilijikuta ikipoteza robo tatu na kutoka sare moja kwa kufungwa 5-4, 12-8 na 16-22 na ile ya mwisho 7-7.

Jitegemee leo itashuka tena dimbani katika netiboli kucheza na Shimba Hills ya Uganda kabla ya kucheza mchezo wa mwisho dhidi ya dada zao wa Kizuka pia ya Tanzania.

Katika mchezo mwingine wa netiboli jana, St Marys Kitende ya Uganda iliibuka kifua mbele dhidi ya Kibuli kwa bao 40-20, huku LTP Bujumbura ya Burundi ikipokea kisago cha bao 78-7 kutoka kwa Kizuka ya Tanzania katika mchezo uliotawaliwa na washindi.

Katika mpira wa kikpau, Bujumbura iliibuka na ushindi mnono baada ya kuwachapa Kizuka ya Tanzania kwa pointi 75-40 huku katika mpira wa wavu GSI ya Rwanda iliibuka na ushindi wa seti 3-0 dhidi ya Mary Hills ya Uganda.

Katika mchezo mwingine wa mpira wa wavu, Bisunga ya Uganda iliishinda AIC Hills ya Uganda pia kwa kuifunga seti 3-0 katika mchezo uliofanyika nje ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika soka, timu ya Makongo Sekondari ilishindwa kutamba mbele ya Mvala ya Uganda baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo mkali uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.

MKOA wa Pwani umeanza kwa kishindo maandalizi ya kushiriki mashindano ...

foto
Mwandishi: Cosmas Mlekani

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi