loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JK ahimiza ushirikiano kukabili tabia nchi

Rais Kikwete amesema hayo juzi mjini Malabo, Equatorial Guinea wakati akifungua Mkutano wa Wakuu wa Nchi 11 zinazounda Kamati ya Mazingira ya Nchi za Umoja wa Afrika(CAHOSCC).

“Suala la Tabia Nchi barani Afrika ni changamoto na fursa pia kwani kama tukifanya uamuzi mzuri tunaweza kupata manufaa kutokana na mbinu mbalimbali zilizopo za kupunguza madhara yake”alisema.

Rais Kikwete alizitaka nchi kulichukulia suala la Tabia Nchi kwa umakini mkubwa kwani kwa hali iliyofikiwa hivi sasa, hakuna chaguo lingine bali kuangalia njia za kupunguza athari zake.

Nchi wanachama wa Kamati ya Mazingira ya AU in Tanzania ambaye ndiye Mwenyekiti, Algeria, Ethiopia, Congo-Brazaville, Kenya, Mauritania, Mauritius, Msumbiji na Uganda.

Kamati ya Mazingira ya AU ina jukumu la kuongoza nchi za Afrika katika kupanga mikakati, mbinu na njia mbalimbali za kukabiliana na madhara ya Tabia Nchi barani na pia kuzitumia changamoto zake katika kuleta maendeleo na matokeo chanya katika jitihada hizo kwa manufaa ya nchi za Afrika.

Kamati ya AU imesisistiza kuwa nchi za Afrika zinahitaji kuboresha uwezo wake wa kupata taarifa za tahadhari katika ngazi zote, uwezo wa kifedha, mawasiliano na usafirishaji katika miji yake na pia kuongeza uwezo wake wa kuzuia mafuriko kwa kutumia njia za kisasa, uwezo wa kupanga miji na kupunguza athari za sasa na baadaye kwa ajili ya wananchi wake na uchumi pia.

Alisema pia bara la Afrika linahitaji elimu na maarifa zaidi kwa wananchi wake kwa ujumla kuhusu athari hizi na tahadhari kwa ujumla.

RAIS John Magufuli amewataka wasaidizi wake ...

foto
Mwandishi: Mwandishi wetu, Malabo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi