loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JK azindua kijiji cha mfano cha vijana

Baada ya kuwasili jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Tabora, ambao umejengwa upya na kisasa, Rais Kikwete alikwenda moja kwa moja kwenye kijiji hicho kilichopo kilomita 60 kutoka mjini Tabora kufanya shughuli yake ya kwanza ya kikazi mkoani Tabora.

Kijiji hicho ambacho tayari kina vijana 70 kilianzishwa rasmi Aprili mwaka jana, kikiwa na vijana 100 kwa lengo la kutafuta njia za kujikomboa kimaisha na shughuli kubwa zinazofanyika kwenye kijiji hicho kwa sasa ni kilimo; ufugaji wa nyuki, ng’ombe na kuku; ufundi sanifu wa uashi na useremala, ushonaji wa sare za shule na utengenezaji viatu.

Aidha, kijiji hicho kinazo shughuli za uchongaji madawati, utundikaji mizinga ya nyuki ambayo imefikia 750, usindikaji wa siagi ya karanga, upasuaji na urandaji wa mbao usindikaji wa asali na usagaji wa unga wa sembe ambao unaitwa Vijana Super Sembe.

Kijiji hicho kinachoendelea kujengwa kwa bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge tayari kina jengo la utawala, karakana ya kisasa, mabanda ya mifugo, ghala na tayari zinajengwa nyumba za kisasa kwa ajili ya makazi ya vijana.

Mpaka sasa halmashauri hiyo imetumia kiasi cha Sh bilioni 1.3. Kijiji hicho cha mfano na cha aina yake nchini kinalenga kuwafundisha vijana namna ya kutafuta njia na mbinu za kujikomboa kimaisha na waanzilishi wake wanataka kukifanya kijiji hicho kuwa Jiji la Kijani.

Akizungumza na maelfu ya wananchi wa kijiji hicho na vijiji vya jirani kwenye mkutano wa hadhara, Rais Kikwete aliwapongeza viongozi wa Mkoa wa Tabora kwa kubuni na kutekeleza wazo la kuanzishwa kwa kijiji hicho.

Aidha, Rais Kikwete aliupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kwa kugharamia ujenzi na uendeshaji wa kijiji hicho.

Aliahidi kukinunulia kijiji hicho trekta moja na pia kutoa Sh milioni 100 kusaidia uboreshaji wa shughuli za kijiji hicho.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Sikonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi