loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Juan Mata kuiokoa Man United?

Ndiyo, United ilikuwa bila ya majeruhi Robin van Persie na Wayne Rooney – lakini kilichoachwa nyuma kilikuwa ni kichekesho, mchezo uliokosa msisimko, kwani Sunderland walistahili kushinda mechi ya marudiano ya nusu fainali ya Capital One baada ya mikwaju ya penalti, katika staili ya kuchekesha.

Haikuwa suala la kuchekesha kwa Moyes kwani msimu wake mbaya alioanza kama mrithi wa Sir Alex Ferguson, ulichukua mwelekeo mbaya tena baada ya kupoteza mechi hiyo kwa Sunderland inayoshika nafasi ya 19 katika Ligi Kuu, hivyo kukosa kukutana na Manchester City katika fainali Wembley.

Moyes alikataa kujibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu usajili huo wa Mata baada ya kipigo – labda kwa kukataa kutabiri hatima ya uhamisho huo huku tayari mambo yakiwa yameshakwenda kombo.

Lakini United na mashabiki wake waliachwa wakisubiri tumaini la kumpata kiungo huyo wa Hispania, mara baada ya kukumbana na usiku mwingine mbovu Old Trafford.

United ilionekana kama timu inayohitaji ubunifu na upiganaji wa kutisha wa Mata. Kwa hiyo, ni masuala gani yanayozunguka usajili wake? Mata amenunuliwa kwa kupaniki?

Mmoja wa wachambuzi katika Old Trafford alisema kabla ya mechi: “Ndiyo, Mata amenunuliwa kwa kupaniki – lakini ni mchezaji mzuri aliyenunuliwa kwa kupaniki (kuchanganyikiwa).”

Kelele zote zilizokuwa zikipigwa msimu huu kwa United ni kwamba hawakuwa na haja ya mchezaji kama Mata au Mesut Ozil kwa sababu wanaamini wana wachezaji mahiri katika eneo hilo, kwa wachezaji kama Wayne Rooney, ambaye anaweza kucheza nyuma ya mshambuliaji, Adnan Januzaj au hata Shinji Kagawa katika nafasi ya “namba 10.”

Malengo yalikuwa ni namba tatu, kiungo wa kati wa ukweli na pia uwezekano wa kununua mlinzi wa kati. Haya yote yamebadilika. Je, ni kwa sababu ya jinsi walivyofungwa Jumapili iliyopita na Chelsea, wakati kikosi cha Jose Mourinho kiliposukuma mbele mpira na kuifunga moja ya timu zilizoaminia kuwa kiboko?

Au ni uwezekano wa kukosa nafasi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uliosukuma usajili huo wa ghafla? Kumekuwapo na mijadala kuwa United inaweza kupita msimu mmoja bila ya kuwamo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hii ni hatari kwa sababu ukiwa nje hakuna uhakika wa kurejea msimu unaofuata. Liverpool walifikiria kuwa watakuwa nje kwa msimu mmoja baada ya kukwama mwaka 2010, lakini hawajarejea, na kuwasili kwa Mata kuna maana ya kuhakikisha United wanaepuka balaa hilo.

Labda ilikuwa ni kwa sababu ya kununua mchezaji wa kiwango cha juu aliyekuwapo, bila ya kujali dau kubwa, na fursa ilikuwa nzuri kutoipoteza. Kuchanganyikiwa ni neno kali sana, lakini kuna mshangao fulani kuhusu kasi ya uhamisho huo wa United na nafasi waliyoamua kuwa kipaumbele na kutumia mamilioni ya fedha. Je, Manchester United inamhitaji?

Tazama kipigo kutoka kwa Sunderland. Katika utetezi, Moyes alisema hakuwa na Rooney na Van Persie, lakini ukiondoa Januzaj, United ilikuwa zaidi ya neno ambalo halikuwa likitajwa wakati wa Sir Alex Ferguson – goigoi.

Moyes atakuwa na kazi ya kumpachika Mata mwenye umri wa miaka 25 katika kikosi chake ambacho tayari kinaonekana kimejaa, lakini ikiitazama United ilivyohaha kupata makali dhidi ya Sunderland, ilikuwa ni kielelezo kwa nini usajili wa nyota huo una maana. Muhimu kwa Moyes ni kutafuta nafasi sahihi kwa Mhispania huyo.

Yeye si winga na siyo kiungo wa kati, kwa hiyo itakuwa ni jambo muhimu kuona kocha huyo wa zamani wa Everton atakavyomtumia. Hata kwa kuruhusu wasiokuwapo, kufungwa na Black Cats – ambako United ilikuwa nyanya kwa muda mwingi wa mchezo – kunaongeza uzito wa kumnyakua Mata. Kunaweza kuongeza uzito katika timu ambayo ilishinda taji la Ligi Kuu msimu uliopita, lakini Manchester United haina wachezaji wa kutosha wa kiwango cha juu.

Mata ni mmoja wao, United inammudu kigharama na ni bora kuliko wachezaji wengi ilionao. Kwa hiyo, uhamisho wake unafaa. Atatatua matatizo? Labda kama achezeshwe kama kiungo wa kati bora duniani – na hataweza.

Mata ana kipaji cha hali ya juu, waulize mashabiki wa Chelsea ambao wanamhusudu, lakini ni mpambaji mzuri kwa United, kuliko kuwa ufumbuzi wa matatizo yake mengi. Moyes ni lazima atafute wachezaji wa kuziba mapengo yaliyoachwa na Roy Keane na Paul Scholes kwa miaka ijayo. Kuwasili kwa Mata kutaongeza uzito na ubora, lakini kazi kubwa imebaki.

Hiki ni kikosi cha United ambacho kimefifia ambacho kiko kimetolewa michuano ya vikombe viwili vya ndani, ikiwa pointi 14 nyuma ya Arsenal kileleni mwa Ligi Kuu na siyo washindani wa kuaminika katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Inahitaji msaada wote kokote itakapopata. Nani wataathirika?

Usajili wa Mata unaweza kuleta changamoto kwa majina makubwa Old Trafford kwa sababu ya kupenda kwake kucheza nyuma ya mshambuliaji.

Hatima ya Rooney bado imegubikwa na uvumi mkubwa, wakati Van Persie atafikisha miaka 31 mwaka huu na inaonekana amerejea katika matatizo yake ya majeraha ya mara kwa mara baada ya kuwa na msimu mzuri Arsenal na kuipa United taji msimu uliopita.

Moyes anaweza kumtumia Van Persie kama mshambuliaji wake na muunganiko na Mata, Rooney na Januzaj nyuma wakati huo akiteua viungo wawili wakabaji – lakini hili linaweza kuleta taabu. Ni fumbo lisilo na mfumbuzi na linaweza kusababisha Januzaj mwenye umri wa miaka 18 asitumike vyema katika nafasi yake – ingawa bado anahitaji ufundi wa kufanya maamuzi ambao unaendana na kukomaa kiakili – wakati mkataba wa Mata unaonekana kumuathiri Kagawa.

Kuwasili kwa Mata kunaweza pia kuwa mwanzo wa mchakato mkubwa wa kuijenga United utakaofanywa na Mata. Ushahidi wote msimu huu unaonesha kuwa United unahitaji mabadiliko makubwa na hakuna dalili ya kusajili mchezaji ambaye anaweza kuwa tishio na kuendana na Ligi Kuu na hasa mechi kubwa.

Kusajiliwa kwa Mata kutasaidia hilo kwa Moyes na Manchester United. Matukio kabla ya mechi uwanjani na kipigo cha Sunderland, kulikuwa na hali ya kuhuzunisha Old Trafford, kabla ya habari za usajili wa Mata.

Na baada ya kipigo hicho ambacho kimeendelea msimu mbaya kwa kikosi cha Moyes, kulikuwa na angalau faraja kutokana na taarifa za usajili wa Mata.

Ilionesha kuwa United sasa imedhamiria kazi kweli kweli baada ya kukwama katika usajili mwanzoni mwa msimu huu na kutoa uthibitisho kuwa Moyes anaweza kuleta wachezaji mahiri – ingawa Mata amesukumwa zaidi na ukweli kuwa fainali za Kombe la Dunia ziko ukingoni.

Nguvu ya Mourinho Labda shetani katika hili ni Jose Mourinho. Jumapili iliyopita, baada ya kuishinda United, alisema kwa sauti ya huzuni, kwamba United haimo tena katika mbio za ubingwa, lakini akatumaini kuwa itamaliza nafasi ya nne kwa kuwashinda wapinzani wa Chelsea sasa na mwisho wa msimu.

Na njia bora ya kuwasaidia ni kwa kuwauzia mchezaji aliye katika kiwango bora Ulaya, lakini anayeonekana kuwa mzigo Stamford Bridge.

Ni ngumu kumhukumu Mourinho katika hili, lakini kwa akili ya kawaida, ni kwamba anaweza kulitazama hili kwa njia ya kupata donge nono la fedha kwa klabu ambayo anaiona si mshindani wake wa ubingwa kwa ajili ya mchezaji ambaye hamhitaji. Na hili lina maana gani kwa nguvu ya Mourinho na umaarufu wake Chelsea?

Kama, Rafael Benite angeamua kumuuza Mata, na akaamua kumuuza kwa Manchester United, kungekuwa na mapinduzi ya kijeshi na maandamano katika mitaa ya King’s Road. Neno la Mourinho ni sheria na linakubalika.

Ni mtu asiyeguswa. Kama amefanya uamuzi sahihi wa kubariki uuzwaji wa Mata kwa Manchester United, ni suala la kusubiri.

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi