loader
Dstv Habarileo  Mobile
Julio ajitosa uchaguzi Simba

Julio ajitosa uchaguzi Simba

Kati ya hao, watatu ni katika nafasi za Urais na sita Makamu Urais, wakati pazia la uchukuaji fomu hizo linafungwa jana saa 100 kamili jioni, hao ndio waliochukua na kurejesha fomu hizo, huku baadhi wakirudisha kwa mbwembwe za kusindikizwa na mashabiki wao.

Kwa mujibu wa Katibu Msaidizi wa Kamati ya Uchaguzi Simba, Khalid Kamguna, waliojitokeza kuwania nafasi ya Urais ni Evans Aveva, Michael Wambura na Andrew Tupa.

Idadi hiyo ukilinganisha na waliojitokeza uchaguzi uliopita ni tofauti kidogo kwani mwaka huu wamepungua kutoka sita hadi watatu. Katika nafasi ya Makamu Urais ni sita ambao ni Wilbert Mayage, Joseph Itang’are, Swedi Mkwabi, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, Bundala Kabulwa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio.’

Wakati anachukua fomu kwa mbwembwe jana huku akitoa Dola za Marekani 200 (Sh 320,000) kwa ajili ya kununua fomu hizo, Julio alisema ameamua kuwania nafasi hiyo kwa vile anaipenda Simba na ndiye kocha mwenye mapenzi ya kweli kwa klabu.

Alisema wakati Kamati ya Utendaji ikiongozwa na Kaimu Makamu wa Rais, Joseph Itang’are ikiwafukuza na baadhi ikiwazomea, bado hakukata tamaa kwa sababu anaipenda Simba.

Pia alisema katika uongozi wa Hassan Dalali alikuwa akiudai Sh milioni 24, lakini hakuzidai kwa sababu alijua ndiye mwenye Simba, lakini ameupeleka uongozi uliopita mahakamani kutokana na kumdhulumu.

Waliojitokeza katika nafasi za ujumbe ni 32 ukilinganisha na Uchaguzi Mkuu wa 2010 ambao wagombea walikuwa 24, kwa hiyo idadi ya mwaka huu imeongezeka.

Wanaowania ujumbe ni Damian Manembe, Ally Chaurembo, Ibrahim Masoud, Ahmed Mlanzi, Idd Mkambala, Kessy Kikoti, Abdulhamidu Mshangama, Amina Poyo, Alfred Elia, Ally Suru, IddyNoor Kajuna, George Wakuganda na Said Tully.

Wengine ni Ramson Rutiginia, Seleman Dewji, Khamis Mkoma, Said Pamba, Rodney Chiduo, Collin Frisch, Chano Hassan, Emmanuel Kazimoto, Juma Pinto, Salum Jazaa, Yassin Mwete, Hussein Simba, Asha Muhaji, Asha Kigundula, Maulid Abdallah, Juma Musa, Omar Said, Said Kubenea na Jasmin Sudi.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi