loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

K-Mondo yajisogeza kwa mashabiki

Akizungumzia ziara hiyo katika Jiji la Dar es Salaam, Msemaji wa bendi hiyo, Richard Mangustino alisema kwanza ni kuimarisha ngome ya mashabiki wa bendi hiyo inayotarajia kuzindua albamu yake Aprili mwaka huu, lakini kingine, ni kutambulisha nyimbo zake mpya kwa mashabiki kabla ya kwenda redioni.

Mangustino alisema bendi yao ina muziki mzuri na wanamuziki wengi wazuri ambao wangependa mashabiki wao wawaone ili wapate burudani ambayo wamekuwa wakiikosa katika kipindi kirefu.

“Bendi yetu imepata uongozi mpya ambao umeamua kuwafuata mashabiki wa K-Mondo kule kule wanakoishi na ndio maana wiki hii tutakuwa Kariakoo na wiki ijayo tutakuwa Kibaha ambako tutahakikisha wapenzi wa K Mondo huko wanapata burudani nzuri,” alisisitiza Mangustino.

Moja kati ya mambo ambayo bendi hiyo itafanya ni pamoja na uzinduzi wa nyimbo zao mbili jukwaani; Kidole Gumba na Sema na Mimi, ambazo zote zimeimbwa katika mtindo wa dansi. Nyimbo nyingine kali ambazo zitatambulishwa kwa wapenzi wa Kariakoo ni pamoja na Njiwa, Nelly, Sharufa, That Day na Magambo.

Klabu ya Liverpool na Manchester United zipo vitani kumuwinda ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi