loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kada atoboa siri ya migororo UVCCM Arusha

Pia vijana hao hung’ang’ania kuingia katika jumuiya hiyo kwa maslahi yao na sio kama kweli wanamapenzi mema na CCM.

Kauli hiyo imetolewa na kada mkongwe wa CCM jijini Arusha, Modest Meikoki katika mahojiano maalumu na gazeti hili.

Alisema migogoro mingi ya kiutendaji ndani ya UVCCM inayotokea Arusha inachangiwa na maslahi binafsi pamoja na makundi ya urais 2015 kitu ambacho ni hatari.

Meikoki ambaye alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arusha kwa zaidi ya miaka 10 kuanzia mwaka mwaka 1986 na mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ya Arusha kwa miaka 26, alisema vijana wa sasa ambao hujiita ‘’kizazi kipya’’ ni tatizo katika uongozi kwani wengi wao hupitia jumuiya hiyo kutaka uongozi serikali na sio kujenga chama.

Alisema ili kuondoa migongano na migogoro ndani ya UVCCM Mkoa wa Arusha viongozi wa juu wanapaswa kuwakemea wahusika na kuwaeleza ukweli katika vikao ikishindikana wachukuliwe hatua ikiwa ni pamoja na kufukuzwa chama.

Meikoki ambaye pia aliwahi kushika wadhifa wa Unaibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa (sasa Jiji) Arusha kwa miaka miwili na udiwani miaka mitano katika kata ya Daraja Mbili, alisema vijana wengi wa UVCCM Mkoa wa Arusha ni wanafiki na wanafuata mkumbo kwa kila kitu bila ya kutafakari kwa maslahi yao.

ABIRIA 80 wakiwemo watalii wameshuka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi