loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kalambo kuwania kombe, jezi

Kwa mujibu wa Katibu wa KLFA, Bonivenure Feruzi, ligi hiyo itakayofikia kilele chake siku ya maadhimisho ya sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 9, mwaka huu, itazishirikisha timu 17 kutoka kata zote.

Hayo yalibainishwa hivi karibuni na Feruzi wakati wa uzinduzi wa kuanza kwa ligi hiyo uliofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Moshi Chang’a mjini Matai ambayo ni makao makuu ya wilaya hiyo.

Alibainisha kuwa michuano hiyo inayodhaminiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Rukwa, Rosweeter Kasikila, itafanyika kila mwaka na kulenga kukuza vipaji vya mchezo huo kwa vijana wa kiume na pia wa kike kutoka ngazi za vijiji.

Kwa mujibu wake, ligi hiyo iliyoanza Juni mwaka huu katika ngazi za kata ambapo vijiji husika vya kila kata vilichuana na kupata wachezaji bora waliounda timu moja ya kata itahitimishwa kwa mshindi wa kwanza kupata kikombe kikubwa jezi na fedha taslimu Sh 300,000.

Mshindi wa pili atazawadia kikombe na Sh 200,000 ambapo wa tatu atajinyakulia kikombe na Sh 100,000.

Pia itaundwa timu moja ya kombaini ya wilaya itakayokuwa chini ya uangalizi wa KLFA katika masuala ya ufundi utaalamu na maslahi ya wachezaji.

Awali, mgeni rasmi, DC Chang’a alizindua ligi hiyo kwa kutengewa mpira wa penalti na kufunga bao, alisema Serikali wilayani humo itaendeleza utaratibu wa kuyatumia mashindano ya aina hiyo kwa ajili ya kuchagua wachezaji wazuri watakaoshiriki mafunzo ya mchezo huo chini ya kocha mwenye ujuzi na kujenga hamasa kwa wadau wa soka wilayani humo kuchangia michango yao ya hali na mali.

MBIO ya Tanzania Women ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Kalambo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi